CRISTIANO Ronaldo nyota wa kikosi cha Juventus atasalia ndani ya kikosi hicho licha ya kuelezwa kwamba Real Madrid na Manchester United wanahitaji saini yake.
Msimu uliopita nyota huyo ilibaki kidogo asepe kwa kuwa alikuwa anatajwa kuelekea Manchester United ambao walikuwa wanatajwa kuiwinda saini ya nyota huyo.
Wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes inaelezwa kuwa ameomba nyota huyo aongezewe mkataba ndani ya kikosi hicho cha Juventus.
Mkataba wake ndani ya Juventus umebakiza mwaka mmoja kwa kuwa alisaini dili la miaka mitatu akitokea Real Madrid na Mei mwaka huu ilikuwa inelezwa kuwa alikuwa anafanya mazungumzo na Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjaer ili amrudishe ndani ya Old Trafford.
Msimu uliopita raia huyo wa Ureno alifunga jumla ya mabao 36 katika mechi 44 ambazo alicheza ndani ya Juventus.
0 COMMENTS:
Post a Comment