HAJI Omari Mpili, maarufu kama Mzee Mpili amesema kuwa hawezi kushindana na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kwa kuwa ni mtoto mdogo na lazima ataifunga tena Simba watakapokutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Mzee Mpili amebainisha kuwa ushindi wao wa Julai 3 yeye alikuwa ni mchezaji namba moja kwa kuwa ana watu hivyo hana mashaka na mchezo wao kuelekea Julai 25 na amesisitiza kwamba lazima alipwe mkwanja ambao aliahidiwa na Manara ambao ni milioni moja.
"Mimi ninasema kwamba mchezo wetu ule pale taifa nilikuwa mchezaji namba moja na kuelekea kwenye mchezo wetu Kigoma nina amini kwamba nitaucheza na tutashinda.
"Siwezi kushindana na Manara, yeye ni mtoto mdogo haniwezi na mimi nina watu wakubwa kila mahali, sasa ninasema hivi kwa kuwa aliniahidi atanipa milioni moja ninaitaka.
"Yeye mwenyewe Manara alisema kuwa ohh Mzee Mpili ukitufunga sisi nitakupa milioni moja, basi sikumuomba mwenyewe amesema naitaka milioni moja yangu na ninasema kwamba Kigoma tunashinda tena," amesema.
Katika mchezo wa Julai 3, Simba ilishuhudia dk 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga na bao pekee la ushindi lilifungwa na Zawad Mauya dk 12.
Dahh!!!! Jamani imetosha na huyu mzee Mpili......khaaaaa!
ReplyDeleteBora yeye mwenyewe anekiri kuwa alikuwa mchezaji namba moja, hata like shuti alipiga yeye kupitia uchawi wake, ndio alimfumbaza refa asione penati zile, ndio alikuwa golini anapeperusha na kudaka mashuti ya wachezaji wa simba. Kweli uchawi duniani upo. Kimpira utopolo hana uwezo wa kuifunga simba.
ReplyDeleteKama u naamini katika hilo ushafilisika kiakili
DeleteYaani huyu jamaa amekomalia suala la uchawi hadi kichwa kinamuuma...Nina wasiwasi hata mafanikio ya majirani zake mtaani anayaonea wivu na kuwaendea kwa waganga kutokana na jinsi anavyoonesha kuuabudu uchawi.Kama anadhani uchawi ndio suluhisho basi awasaidie Simba kupanga tunguri uwanjani zicheze.Ukishakuwa na imani tele kwenye nguvu za giza usitegemee maendeleo yoyote
DeleteKweli kabisa
DeleteWatu wanasema eti mashuti waliopiga simba, kwani walipiga mangapi?
DeleteShot on target
Simba 2 na Yanga 4
(PAMOJA NA GOLI)
Shot off target
Simba 4 na Yanga 6
Coner
Simba 6 na Yanga 5
Offside
Simba 0 na Yanga 1
Yelow card
Simba 2 Ynga 3
Foul
Simba 21 na Yanga 12
KWENYE HILI ONYANGO NA WAWA WANAJUA, WE BONGO LALA ANGALIA TAKWIMU YALIYOLENGA LANGO 2 TU, USISAHAU ZANZIBAR
SHOT ON TARGET
SIMBA 0 YANGA 13
KAJIFUNZE AU KAANGALIE MARUDIO
Usione aibu kuweka ball possession
DeleteBall possession sio kigezo pekee cha timu kuwa bora katika mchezo husika,inategemea pia na mbinu za timu pinzani katika game approach
DeleteMechi kati ya Kaizer Chiefs na Simba mpaka dk 70 ball posession ilikuwa simba 69 kaizer chief 31 ila magoli yalikuwa simba 0 kaizer 3
ReplyDelete