July 7, 2021

“YANGA imerudi.” Ndivyo ambavyo kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi anatamba baada ya kurejesha fomu ya ushindi ya kikosi hicho, huku akiendeleza rekodi ya Yanga kutopoteza mchezo wowote dhidi ya Simba, katika michezo minne iliyopita ya Ligi Kuu kupitia ushindi wa bao 1-0 walioupata Jumamosi.

Yanga Jumamosi iliyopita walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mpinzani wao wa jadi Simba, katika mchezo wa kiporo cha Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Ushindi huo umewafanya Yanga kufikisha pointi 70 zinazowaweka kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Bara, baada ya kucheza michezo 30.

Akizungumzia kiwango cha timu yake kocha Nabi amesema: “Nafurahi kuona kikosi changu kimekuwa na muunganiko mkubwa tena ndani ya muda mchache ambao nimekuwa nao.

“Bila shaka hii inamaanisha Yanga sasa imerudi, na kadiri tutakavyokuwa pamoja nina matumaini makubwa kuwa msimu ujao tutakuwa na matokeo bora zaidi.”

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said kuhusu mipango yao msimu ujao amesema: “Kwa sasa tumejizatiti kuhakikisha tunamaliza vizuri Ligi Kuu, na kushinda kombe la Shirikisho, halafu tuanze rasmi kujipanga na msimu ujao.

“Lakini niweke wazi kuwa sisi kama GSM tumetenga dau kubwa la usajili wa nyota wapya, tunataka kutengeneza timu bora si tu kwa mashindano ya ndani, bali timu itakayofanya vizuri na kuweka rekodi kimataifa.”

9 COMMENTS:

  1. MWAMBIENI ATUNZE AKIBA YA MANENO, MAANA HAJUI KUWA AMELETWA KUIFUNGA SIMBA LAKINI HAMNA TIMU YA USHINDANI IPO TIMU KAMA TIMU. TAREHE 25 NADHANI ATAELEWA KWAMBA TIMU BORA HAITENGENEZWI KWA AJILI YA DERBY ILA KWA AJILI YA KILA MECHI

    ReplyDelete
  2. acha maneno yako mtani bwana hahahahaaa niombee nikae vizuri ili tushindane vizuri na mpira wetu pamoja na ligi yetu ikue au sio mtani

    ReplyDelete
  3. IMEVUJA: Julai 25 mtu anapigwa 4G

    ReplyDelete
  4. Hiyo stori yote ni ta kuwafunga simba ndio kila siku ndio hiyo hadi siku ya fainali ndio itakwisha

    ReplyDelete
  5. Kila mwaka inarudi mnaanza tambo mapema halafu baadae mnaanza kulaumu tff na bodi ya ligi na kutishia kususia ligi.... Jipangeni acheni maneno mpira unacheWa uwanjani sio mdomoni

    ReplyDelete
  6. Mpira unachezwa uwanjani hata @Manara amelitambua hilo, sasaiv atajifunza kukaa kimya wakati wanaume wakicheza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanaume wakicheza kimataifa wakiwa na uzi wao mwekundu,wewe endelea kushangilia kuifunga simba,kwa taarifa yako jana al ahly kapigwa kwenye ligi yao na timu ya mkiani tena mbili bila,mjomba acha kukariri.mpira ndivyo ulivyo.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic