July 17, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi matarajio yao ya ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Simba, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

Yanga wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliokuwa wa nusu fainali ya michuano hiyo, msimu uliopita.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Hersi alisema kuwa kuelekea katika mchezo huo, watahakikisha wanashinda.“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wetu wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, muhimu katika mchezo huu ambao ni wa fainali ni kubeba taji hilo.

 

“Siku zote tunasema kuwa fainali haichezwi bali fainali hushindwa, hivyo kuelekea katika mchezo huo, tunaenda kwa ajili ya kushinda fainali hiyo,” alisema kiongozi huyo.


Yanga watacheza fainali hiyo wakiwa wametoka kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu, wiki mbili zilizopita.

4 COMMENTS:

  1. Vipi Manji hatajwi tena au alikuja kudhihaki na kutoweka.

    ReplyDelete
  2. Hivi wewe mkia unadhani sisi tunauza dengu,subiri Kigoma na kumbuka mmekuwa mkicheza mechi zote za Fa Dar sisi zote Mikoani Sasa mjiandae kupasuliwa mshono wa pili

    ReplyDelete
  3. Nyie utupolo au ngedere fc mechi zenu nyingi mnafunga Simba kwa kubebwa angalia Ile ya mbili mbili kwa faulo ,penalty mnajidodondosha pia refa wetu wabovu Sana ila ikichezeka kwa haki mtalia Sana nyie na kutaka kupigana uwanjani team mnacheza Kama prison mnakamia tafikiri nyie ni watoto tulishtuka siku Ile hamna jipya zaidi ya rafu na kuroga ngedere nyie

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo kwa wenzenu mnaliona hilo ila kwenu wala hamlioni hilo kuwa Tifu Tifu Wana wa beba pale au Una tafuta kiki kwa piki piki tulia dawa imuingie na tarehe 25 cjui mtaweka wp hizo sura zenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic