July 19, 2021

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kimeanza safari ya kureja Dar leo Julai 19 baada ya kukamilisha mzunguko wa pili.

Jana kilikuwa Dodoma, makao makuu ya Tanzania hivyo leo watakuwa kwenye mji mkuu wa biashara, Dar.

Msimu wa 2020/21 Yanga imeufunga kwa kugawana pointi mojamoja na Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa jana Julai 18, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na ulikamika kwa sare tasa.

Kikosi hicho kinarejea kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Simba ambao ni wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili na imekusanya jumla ya pointi 74 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.

Itachezwa Julai 25, Kigoma Uwanja wa Lake Tanganyika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic