KOMBE la Shirikisho (CAF) Klabu ya Azam FC ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika hatua ya awali itakutana na klabu ya Horseed FC kutoka nchini Somalia.
Leo Agosti 13 Caf imechezesha droo ya mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho nchini Cairo.
Mshindi wa mtanange huo atakutana na matajiri wa Misri Pyramids FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Azam FC inayonolewa na George Lwandamina ina kibarua kikubwa katika kupeperusha bendera ya Tanzania katika kuifanya Tanzania kuzidi kupasua anga la kimataifa.
Pia wawakilishi wengine katika Kombe la Shirikisho kutoka Tanzania ni Biashara United ambao watamenyana na DIKHIL.
Mechi za awali zinatarajiwa kupigwa Septemba 10-12.
Njia nyeupe kwa Simba.Kikubwa kujipanga kidawasawa tu.
ReplyDeletetunawatakia azam wafike mbali sana vichapo kwenda mbele
ReplyDeleteHiyo picha inaonyesha ugaidi wa Eli Sasi akiwanyima Penat AZAM
ReplyDeleteSisi mtuombee msituombee tunapiga hata tungepangiwa Nani Mwananchi anajambo lake. Up
ReplyDelete