August 17, 2021


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kwamba kwa sasa umefunga majalada yote yanayohusu usajili kwa ajili ya nyota wapya watakaotumika kwenye kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin alisema kuwa kazi kubwa waliofanya ni kusajili wachezaji ambao ni mapendekezo ya kocha na kwa sasa zoezi hilo limekamilika.

 

“Kuhusu masuala ya usajili kwa sasa sisi tumeshafunga kwani hapo awali tulikuwa tunahitaji kuweza kutumia mashindano ya Kagame kupata wachezaji lakini tumekamilisha zoezi letu.

 

“Tumefanya usajili mzuri hasa ukizingatia kwamba tunakwenda kushiriki mashindano ya kimataifa na ligi hivyo malengo yetu ni kuona tunafanya vizuri katika mashindano yote ambayo tutashiriki,” alisema Amin.

 

Usajili uliokamilika na kutangazwa na Azam FC ni wachezaji saba ambao ni kipa Ahmed Ali Suleiman ‘Salula’ kutoka KMKM, Edward Manyama beki kutoka Ruvu Shooting, kiungo mkabaji, Paul Katema, Charles Zulu kiungo kutoka Cape Town, Kenneth Muguna kutoka Gor Mahia, Rodgers Kola kutoka Zanaco na Idris Mbombo kutoka El Gouna ya Misri, hawa ni washambuliaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic