KLABU ya Azam FC leo Agosti 14 imezindua rasmi nembo mpya, (logo) ambayo imeanza kutumika leo baada ya uzinduzi.
Zoezi la uzinduzi wa nembo hiyo limefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena, Dar na ilihudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Katibu Mkuu wa TFF, Walllace Kidao pamoja na familia moja ya timu kazi ya Azam.
Zoezi la uzinduzi wa nembo mpya ya Azam FC, limezinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulalim Amin, amesema kuwa lengo kubwa la kufanya mabadiliko hayo ni kwenda na kasi ya mafanikio huku malengo makubwa ikiwa ni kuifanya timu hiyo izidi kujulikana zaidi.
Akizungumza kuhusu nembo hiyo baada ya uzinduzi, Bashungwa amesema kuwa ni moja ya nembo nzuri na anawapongeza Azam FC kwa hatua ambayo wamefikia huku akizitaka timu nyingine kuiga suala hilo.
Pia ameongeza kuwa Serikali ipo bega kwa bega na sekta ya michezo pamoja na Waandishi wa Habari kwa kuwa kazi nimoja kufikia malengo kwenye sekta zote.
Ipo Bomba
ReplyDeleteWale jamaa zetu nao wabadili maana Ile yao ina mapicha picha ya ugomvi
ReplyDeleteWabadilishe na mtazamo pia, Azam mara zote wanaumia gharama kubwa kusajili lkn wachezaji hawa delivere kama Yanga na Simba, lkn wachezaji watoe heshima ya thamani halisi ya Azam Fc,
ReplyDeleteKila msimu kushika nafasi ya 3 haipendezi