Nyota huyo ni kijana ambaye ana miaka 24. Taratibu zote za usajili zimefikia pazuri na atajiunga na timu Morocco.
Pape Ousmane Sakho (24) ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Senegal akiwa na Teungueth walitwaa ubingwa wa ligi.
Kiungo huyo mshambuliaji anatajwa kuwa mchezaji wa ndani mwenye kipaji kikubwa nchini Senegal.
Ni mabao 8 na pasi 10 alitoa , pia ndiye mchezaji aliyeng'ara wakati timu ya Teungueth ikiitoa timu ya Raja Casablanca ya Morocco msimu ulioisha na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League.
Kwa sasa Simba ipo nchini Morocco kwa ajili ya kambi ya msimu wa 2021/22.
Leta majembe tuendelee kutwaa ubingwa
ReplyDeleteKwakweli wanatisha Simba. Wataanguka watu chali kabla ya kupigwa mateke
ReplyDeleteEndeleeni kuota ndoto as mchana mpaka mkamrudisha Ajibu na wengine..hehe
ReplyDeleteNafurahishwa zaidi na usajili wa simba msimu huu yaonekana kila siku zikienda mbele wanaohusika na usajili ndani ya Simba huwaga wanajifunza kitu. Peter Banda miaka 20,sakho24, Nyoni 24,muhilu,mwenda Israeli,Kibu, nakadhaika hawa ni wachezaji wenye vipaji vikubwa kwa hivyo uwezekano wa timu kuja kunafuika mara mbili ni mkubwa kwa maana yakwamba ya kuipa Simba mafanikio ya uwanjani ni mkubwa kwakuwa ni vijana Wana Nguvu lakini pia biashara, hawa vijana wakitiki basi umri wao utawavutia wengi wenye pesa zao watakaokuja kutaka kufanya nao kazi.
ReplyDeleteHao kina Israel Mwenda, Kibu n.k, wataishia kupelekwa kwa mkopo timu ndogo kama Namungo. Tukumbuke akina Salamba, Kaheza, Ame, Duchu walikoishia!
Deletehata kama ni chama asingejituma angepekwa tu.................wajitume
DeleteTimu ikisajili inaitwa ina sifa, ikitwaa ubingwa refa wanapendelea, ikiuza wachezaji oooohh mmeishiwa sasa sijui hawa ndugu niwaitaje? Haya semeni ninyi Simba wafanye nini?
ReplyDelete