KLABU ya Barcelona inavutiwa na uwezo wa nyota wa Arsenal, raia wa Gabon, Pierre Emerick Aubameyang ambaye ni nahodha wa kikosi hicho pia jambo linalowafanya wafikirie kuinasa saini yake.
Vigogo hao wa La Liga wapo tayari kumtoa mchezaji wa zamani wa Liverpool ambaye ni kiungo, Philippe Coutinho ili iwe sehemu ya kukamilisha dili la kumpata Auba mwenye miaka 32 na mkataba wake wa miaka mitatu ndani ya timu hiyo unaishi mpaka 2024.
Aubameyang, alijiunga na Arsenal kwa dau la Euro milioni 60 Januari 2018,msimu uliopita alitupia jumla ya mabao 14 chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta na timu hiyo haitashiriki mashindano ya European kwa mara ya kwanza baada ya kuyeyusha miaka 25 kwa kuwa ilikosa vigezo.
Barcelona walijaribu kuisaka kwa udi na uvumba saini ya mshambuliaji Tammy Abraham mwenye miaka 23 kutoka Chelsea, ila dili lao lilibuma kwa kuwa nyota huyo alikamilisha uhamisho wake ndani ya Serie A katika Klabu ya Roma kwa dau la Euro milioni 34 hivyo nguvu zao zote ni kwa Auba.
0 COMMENTS:
Post a Comment