August 2, 2021


 UONGOZI wa Yanga leo umemtambulisha nyota mpya mwingine ambaye atakuwa ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/21 ikiwa ni baada ya jana Agosti Mosi kumtambulisha mshambuliaji Fiston Mayele ambaye amepewa jezi namba 9.

Ni Yusuph Athuman kutoka Biashara United ambaye ametambulishwa leo rasmi kwa dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Taarifa rasmi kupitia ukurasa wa Instagram wa Yanga imeeleza kuwa kwa sasa Yusuph Athuman ni njano na kijani.

Nyota huyu ni mshambuliaji ambaye yupo kwenye timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20.

11 COMMENTS:

  1. Kumekucha huko mjiandae kisaikolojia msimu huu makombe yote tunabeba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata msimu huu mlisema zote zenu. Kambebeni injinia sio makombe

      Delete
  2. Naye mtamwona CECAFA siyo Mayele au DJuma,Makambo,nk bila kusahau ????????

    ReplyDelete
  3. Tunategemea mazuri kutoka kwao

    ReplyDelete
  4. Mdogo wangu Joseph unajiunga timu hii Shaolin soka unaiweza lakini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bora amejiunga na Shaolin soka kuliko kujiunga na watembea uchi hadharani

      Delete
  5. Alitusumbua Sana kweli hapa Kocha tumepata

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic