August 14, 2021


 DITRAM Nchimbi nyota wa timu ya Yanga anatajwa kuwa kwenye rada za Biashara United ambao wanahitaji kupata saini yake.

Biashara United inashiriki Kombe la Shirikisho msimu huu na ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi chake.

Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kutua hapo ni pamoja na Nchimbi ambaye msimu wa 2020/21 aliweza kutupia bao moja ilikuwa mbele ya Gwambina FC.

Kuhusu tetesi ya yeye kutakiwa kuondoka Yanga alibainisha kwamba anaziona kwenye mitandao huku yeye akitambua kwamba ni mali ya Yanga.

"Mimi nipo Yanga na nimekuwa nikiskia kwamba kuna timu ambazo zinanihitaji hilo mimi sijui. Sifikirii kuondoka Yanga kwenda timu nyingine kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Yanga," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Nakushauri wende zako Biashara ukihisi hawakutaki kwasababu unaweza kutimuliwa yanga wakati kila kitu kimemalizika ukabaki hupo yanga huko Biashara huko kokote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic