RAJAB Athuman nyota anayecheza ndani ya timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 alikuwa ni nyota wa mwisho kwa timu hiyo kupiga penalti ambayo ilileta ushindi kwa taifa la Tanzania mbele ya Burundi kwenye fainali ya Cecafa, nchini Ethiopia.
Nyota huyo amebainisha wazi kwamba penalti zina presha kubwa ila wanashukuru Mungu kwa kuwa wameshinda taji hilo. Tanzania ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya dakika 90 ngoma kuwa Tanzania 0-0 Burundi.
Kutokana na ushindi huo jana Agosti Mosi baada ya kurejea Tanzania, Rais Samia Suluhu naye alituma salamu za pongezi kwa U 23 kutwaa taji hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment