IKIWA kwa sasa timu zipo kwenye hesabu za usajili tayari mabosi wa Azam FC wamemalizana na nyota sita kwa ajili ya msimu ujao.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo ulikuwa ni utambulisho wao wa mwisho hivi karibuni ambapo bado wapo sokoni kusaka wacezaji wengine na aliibuka hapo akitokea El Gouna ya Misri.
Nyota wote ambao wamemalizana na Azam FC madili yao walisaini mbele ya Abdulkarim Amin 'Popat', ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Azam FC.
Ataungana na mshambuliaji namba moja wa timu hiyo ambaye ni Prince Dube mwenye mabao 14 na pasi tano kwa msimu uliomeguka wa 2020/21.
Wengine ambao wamemalizana na Azam FC ni nyota watatu kutoka Zambia, Charles Zulu, Paul Katema, mshambuliaji Rodgers Kola, Mkenya Kenneth Muguna na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.
0 COMMENTS:
Post a Comment