August 16, 2021


 KOCHA wa Simba, Didier Gomes, amesema kuwa moja kati ya programu ambayo anaitilia mkazo kwa sasa akiwa Morocco ni wachezaji wake kufunga mabao ya mbali.


Gomes alisema kuna kazi 
nyingi za kufanya akiwa Morocco, lakini kubwa zaidi ni timu kuweza kufunga kwa kila namna ikiwemo nje ya boksi la wapinzani kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na njia nyingi za kupata ushindi wakati wa mechi.


Simba kwa sasa ipo Morocco ilipoweka kambi ya kujiandaa na msimu wa 2021/22 ambapo ipo huko tangu Jumatano wiki hii.


Akizungumzia maendeleo ya kambi hiyo, Gomes alisema kila kitu kinakwenda vizuri kutokana na mazingira yalivyo na kwa sasa wanaangalia namna nzuri ya timu kutimiza kila program waliyoiweka.


"Kambi ipo vizuri kutokana na nchi ambayo tupo hali ya hewa yake kuwa nzuri kwetu, kambi hii ina faida nyingi kwa sasa, tunaagalia zaidi wachezaji kufunga nje ya boksi, tunajaribu kuangalia namna gani vijana watafanyia kazi eneo hilo kwa sasa,” alisema Gomes.


Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara walilotwaa msimu wa 2020/21 baada ya kufunga mabao 78 na kufikisha jumla ya pointi 83.


Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kambi hiyo ni pamoja na kiungo Jonas Mkude na mshikaji wake Taddeo Lwanga, Bernard Morrison, Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga.

4 COMMENTS:

  1. Another thunderous roaring will once more be heard at home and abroad

    ReplyDelete
  2. Ni bora kocha angeweka siri mipango yake ili wasiijuwe wale daima wanaomuiga mnyama kila anachokifanya

    ReplyDelete
  3. Wawa akatafute changamoto shm nyngne ampishe inonga baka 7b umri wake mkubwa sana Wawa ila ametufanyia mamb makubwa wanasimba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic