August 10, 2021

 


REKODI za kipa mpya wa Yanga ambaye amemalizana na timu hiyo Diarra Djigui zinatisha na kwa rekodi zake ni moja kwa moja kipa huyo anaenda kuwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kuelekea msimu mpya wa mwaka 2020/21.

 

Djigui mwenye uraia wa Mali kwa sasa ana umri wa miaka 26 ambapo kipa huyo tayari ameshatua nchini huku tayari akiwa ameshasaini mkataba wa miaka 2 wa kuitumikia Yanga.

 

Mbali na kusaini mkataba huo lakini rekodi za kipa huyo zinatisha  kutokana na mafanikio  makubwa ambayo ameyapata binafasi pamoja na mafanikio ya timu alizozichezea kwa ujumla.

 

Golikipa huyo akiwa na klabu ya stade de Malien ya nchini kwao Mali amefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara tano ambayo ni katika msimu wa mwaka 2012/13, 2013/14, 2014/15, 2015/16 na 2020/21.

 

Pia kipa huyo amefanikiwa kutwaa makombe matatu ya kombe la FA la nchini kwao Mali mara tatu katika msimu wa mwaka 2012/13, 2014;/15 na 2020/21 huku akitwaa kipkombe caha Mali Cup mwaka 2013/14 na 2014/15.

 

Kipa huyo pia katika timu ya taifa  amefanikiwa kucheza michuano ya kimataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN) mwaka 2016 na mwaka 2021 ambapo alikuwa nahodha wa timu hiyo.

 

Lakini pia Djigui alifanikiwa kushiriki michuano ya kombe la dunia chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2015 ambapo kipa huyo alifanikiwa kuliongoza taifa hilo kumaliza katika michuano hiyo wakiwa katika nafasi ya 3.

 

Kuhusu mafanikio yake binafsi Djiugui  amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Mali mara mbili katika msimu wa mwaka 2014/15 nna msimu wa mwaka 2019/20.Lakini pia kipa huyo alifanikiwa kupa kipa bora namba 2 Afrika katika msimu wa mwaka 2014/2015.


5 COMMENTS:

  1. Sema huku ataona mipira miwili miwili asah sijui adake upi

    ReplyDelete
  2. Yetu macho 2 ila icje ikawa kama ya kindoki

    ReplyDelete
  3. Haaaa haaaa,,, umenkumbusha kindoki! Walsema ana mikono buku

    ReplyDelete
  4. Sasa mbona hatujaenda kumpokea kifalme au tunaogopa yasiwe yale yale ya kupokewa kifalme halafu akaondoka kimya kimya

    ReplyDelete
  5. Hili kipa letu jipya lina mikono buku 5 dadadeki mjiandae maana linadaka mpk mipira inayotoka nje yani haliachi kitu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic