WINGA mpya wa Simba, Peter Banda amesema kuwa ameanza kuyazoea mazingira mapya ya klabu hiyo kupitia kwa Bernard Morrison ambaye mara nyingi amekuwa akimchangamsha na kumfundisha namna ya kuzungumza Kiswahili kwa haraka zaidi.
Banda amesajiliwa na Simba katika dirisha hili kubwa la usajili akitokea katika Klabu ya Nyassa Big Bullet ya nchini Malawi ambapo winga huyo anatabiriwa kuja kurithi mikoba ya Luis Miquissone aliyetimka ndani ya klabu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Banda alisema kuwa, ameanza kuyazoea mazingira ya Simba kwa haraka zaidi kutokana na kuchangamshwa na Morrison kwa wachezaji wenzake huku akiweka wazi kuhamasishwa na Morrison kuzungumza Kiswahili huku akianza kumfundisha baadhi ya maneno machache.
“Morrison mara nyingi amekuwa akinitania kupitia wachezaji wa Simba, ghafla nimejikuta nikitaniana na wachezaji wengi jambo ambalo limenifanya niwazoee mapema wachezaji wengi wa Simba, sipo kimya kama mara ya kwanza wakati tunaanza safari ya kuelekea Morroco kwa sasa nimechangamka zaidi.
“Morrison pia amekuwa akinihimiza kujifunza jinsi ya kuongea Kiswahili kwa haraka, mara nyingi huwa ananifundisha
maneno machache ya Kiswahili na mara nyingi nikikosea huwa anafurahi akinihimiza nisikosee, namshukuru sana,” alisema winga huyo.
Safi sana Morrison
ReplyDelete