August 27, 2021


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amefunguka kuwa mpango wake mkubwa ni kuhakikisha wanautumia mchezo wao wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Zanaco FC ya Zambia, kuhakikisha wanafanya vizuri dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

 

Yanga imepangwa kucheza na Rivers United katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kupigwa kati ya Septemba 10 hadi 12, mwaka huu.


Katika mchezo huo, Yanga wanatarajia kuanzia nyumbani, kabla ya kwenda kumalizia ugenini kati ya Septemba 17 na 19, mwaka huu.


Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusu mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United, Nabi alisema: “Tumerejea Dar es Salaam baada ya kuwa na kambi ya muda kule nchini Morocco iliyokuwa na lengo la kutuandaa na msimu mpya, mbele yetu tuna matukio mawili makubwa ambayo tunajiandaa nayo.


“Kuna mchezo wa Kilele cha Wiki ya Mwananchi tutakaocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia.


“Benchi la ufundi tumejipanga kuutumia mchezo huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi dhidi ya Rivers United ya Nigeria.


“Tunawafahamu Zanaco, tunaamini ni kipimo sahihi kwetu kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic