HERITIER Makambo, nyota mpya wa Yanga amesema kuwa anaamini kwamba atafanya vizuri ndani ya timu hiyo kwa msimu mpya wa 2021/22 katika Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dili lake ni la miaka miwili na aliibuka hapo akitokea Klabu ya Horoya AC ya Guinea ambapo huko alisitisha mkataba wake kutokana na kutokuwa na nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Pia Makambo aliibuka huko Guinea akitokea Tanzania kwa kuwa alikuwa akicheza Yanga zama za Mwinyi Zahera ambaye alikuwa ni Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/19.
Wakati anasepa alikuwa ni namba moja kwa utupiaji alitupia mabao 17 ambayo mpaka sasa hakuna mshambuliaji ambaye ameweza kuyafikia kwa kuwa kinara wa msimu huu ni Yacouba Songne mwenye mabao 8.
Yupo kwenye kikosi ambacho kimeibuka nchini Morocco na usiku wa leo kilikuwa Dubai kabla ya kuunganisha safari ya kuelekea Morocco kwa kambi ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.
Makambo amesema:"Nina amini kwamba nimerudi ili kuweza kutimiza majukumu yangu ambayo ni kufunga kwa kushirikiana na wachezaji wenzagu.
"Pia ninapenda kuona tunatwaa makombe kwenye mashindano ambayo tutashiriki hivyo kikubwa ni sapoti na tunaamini kwamba tutafanya vizuri," amesema.
Ikiwa aliondoka kouko kwa kutoonekana anafaa katika kikosi cha kwanza jee huko alipokuwepo sasa wameshapata uchawi wa kumgeuza akawa fit na ikiwa wanao kwanini wasiutumie kurejesha viwango vya Amisi Tambwe, Niyonzima na Ngoma?
ReplyDeleteTuache ushabiki hebu tumuache tusubir tumuone tusihukumu mapema,kwan okwi kard marangap na anaperform,
DeleteUmemjibu vizuri huyo kilaza wa mpira hapo juu
DeleteFact mkuu
DeleteUnamjuwa ajib?
ReplyDeleteKwanza kuandika maneno yenyewe ni mtihani huyo kweli ni bado ana umbumbumbu
DeleteTamy Abraham wa Chelsea ambaye alikuwa hapati namba kikosi cha kwanza mbona amesajiliwa Roma, ko mchezaj kukosa nafasi kikosi cha kwanza inategemea sana mfumo wa mwalimu
ReplyDeleteKuna washabiki wanakariri, Makambo bado yupo vzr ndio maana alikua Horoya FC, time will tell lkn tusiishi kwa mazoea
ReplyDeleteLukaku aliyekuwa man u na yule wa inter milan na leo yupo Chelsea . Utofauti wake nini?
ReplyDelete