August 31, 2021


 MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo ameweka wazi kuwa malengo yake makubwa msimu ujao ni kuhakikisha anafunga mabao mengi zaidi ya 17 aliyofunga kwenye msimu wake wa mwisho alipokuwa Yanga wa 2018/19.

 

Makambo amerejea Yanga akitokea klabu ya Horoya AC ya Guinea, ambapo hii itakuwa mara ya pili kwake kuwatumikia Wananchi, akiwahi kuichezea klabu hiyo kwa mafanikio kwa kipindi cha msimu mmoja wa 2018/19.

 

Katika msimu huo, Makambo alifanikiwa kufunga mabao 21 kwenye michezo 40 ya michuano yote, ambapo kwenye Ligi Kuu Bara pekee alifunga mabao 17.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Makambo alisema: “Najua kuna matarajio makubwa sana ya mashabiki wa Yanga juu ya kikosi chao kwa msimu ujao hasa kutokana na usajili ambao umefanyika, hususani kwa mchezaji kama mimi ambaye tayari wengi wamepata nafasi ya kuniona.

 

“Hivyo najua nina deni kubwa la kuhakikisha ninafunga mabao, kwa sasa siwezi kusema nitafunga mabao mangapi lakini, nataka kufunga mabao mengi zaidi ya mabao 17 ambayo niliyafunga mara ya mwisho nilipokuwa hapa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic