August 6, 2021

 


MSHAMBULIAJI Charles Ilnfya ambaye alipelekwa kwa mkopo ndani ya KMC ili akuze kiwango chake, amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kurudi Simba ili kuendelea pale alipoishia.


Nyota huyo ambaye alipewa dili la miaka 
miwili ndani ya Simba, alikwama kufurukuta zama za Sven Vandenbroeck na alitolewa kwa mkopo kurudi kwenye timu yake ya zamani KMC ambapo huko aliweza kutupia mabao sita na pasi mbili za mabao.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ilanfya alisema kuwa kwa sasa anafikiria kurudi Simba kwa kuwa uwezo anao na anatambua kwamba uwezo wake ni mkubwa.

 

“Nilipokuwa ndani ya KMC nilikuwa ninawasiliana na viongozi kutoka Simba ambapo walikuwa wananifuatilia pia jambo ambalo lilifanya niongeze juhudi.

 

“Kwa hapa ambapo nipo ninaweza kusema kwamba uwezo wa kucheza Simba upo na ninaweza hivyo ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuaje,” alisema Ilanfya.

3 COMMENTS:

  1. Dogo komaa uko uko kmc msimbazi utajisumbua tu hutapata namba na utaua kabisa kipaji chako ushauri nakupa kakaako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni kuwajaza uoga vijana wa kitanzania kujiona kuwa siku zote wao hawawezi.kamwe mchezaji hawezi kuwa bora Kama hajashindana na waliobora. Kwa wenzetu ushindani ni bahati inayoliliwa na kugombaniwa sio kukimbia. Kwa kiasi fulani nafurahi kuona Ilamfia anataka kwenda kupambana ndani ya simba,hakuna kisichowezekana ni kujituma kwa bidii kipaji tayari kipo.

      Delete
  2. Kama kijana anahisi ameshajitambua sawa muache arudi ila Kama bado tia maji basi acha ajiongeze kwanza umri bado unamruhusu.
    Kwa upande mwengine Maoni yangu kwa viongozi wetu wa Simba Kama ujumbe utawafikia basi inatulazimu kufanya usajili wa Funga kazi halafu tuwaache watu waweseke na Manara wao,mchafu wa tabia.
    Tunahitaji wachezaji watatu wa nguvu ili tuwe na jeuri ya kusema tunalitaka kombe la Africa.
    Kama Simba tutasajili Khalid Aucho, Mundele Mukusu,na huyu Beck wa kikongo anaezungumzwa mitandaooni Enock wa mutema pembe basi hakika tutafanikiwa kutengeneza Africa championship Dream team,no doubt.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic