August 2, 2021


 IMEELEZWA kuwa nyota 7 wa Namungo FC ya Lindi huenda wakawa kwenye ile orodha ya wachezaji watakaochwa kwa msimu wa 2021/21 kutokana na kushindwa kwenda na kasi ya timu hiyo.

 

Kwa mujibu wa rekodi za Spoti Xtra inaonyesha kwamba wachezaji hao 7 hawakuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Hitimana Thiery na hata mikoba yake ilipokuwa chini ya Kocha Mkuu, Hemed Moroco hawakuweza kufurukuta.

 

Katika mechi 34 ambazo Namungo ilicheza nyota hao 7 hawakupata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza katika mechi zaidi ya 10 jambo ambalo linayeyusha matumaini yao kubaki msimu ujao ndani ya kikosi hicho.

 

Ni Rodgers Gabriel, Hamis Fakhi, Haruna Shamte, Aman Kyata, Frank Mkumbo, Idd Kipagwile alikuwa kwa mkopo akitokea Azan FC nyota hawa rekodi zinaonyesha kwamba hawajaanza kikosi cha kwanza kwenye zaidi ya mechi 10 kati ya 34.

 

Pia mshambuliaji Adam Salamba huyu rekodi zinaonyesha kuwa hajafikisha mechi tano za kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

 

Katibu Mkuu wa Namungo, Omary Kaaya aliliambia Spoti Xtra kuwa wapo wachezaji ambao watakaochwa ila muda ukifika watajulikana.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic