MSHAMBULIAJI wa zamani wa Klabu ya Yanga, Amis Tambwe amesema kuwa yupo tayari kurudi Bongo ikiwa itatokea timu inamuhitaji ili aweze kusaini.
Tambwe anakumbukwa na mashabiki wa Yanga kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu ambapo alisepa Tanzania msimu wa 2018/19 kutokana na mkataba wake kuisha.
Alifunga mabao 8 kwenye ligi na manne kwenye Kombe la Shirikisho na kumfanya afunge jumla ya mabao 12 ndani ya Yanga wakati akisepa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Tambwe amesema kuwa kwa sasa yupo Burundi akiwa huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu aliyokuwa anacheza nchini Djibout.
“Nipo kwa sasa nyumbani kwa kuwa nilirudi baada ya kumaliza mkataba wangu nilipokuwa nacheza Djibouti la ikitokea timu Tanzania ninaweza kusaini kwani mpira ni kazi yangu,” amesema Tambwe.
Hao wachezaji huru ndo size yetu sisi kwa hiyo tunaomba jembe letu lirudi. Viongozi fanyeni fasta jembe lije tupate makonbe yote msimu huu
ReplyDeleteMpeleke kwa mke wako fasta
DeleteUmri umesha sogea, mechi za ushindani hatoweza, bora aanze kusomee ukocha
ReplyDeleteJamaa daraja la pili inafaa vizuri, timu zilizoshuka mtafuteni huyo jamaa
ReplyDelete