August 27, 2021


 IMEELEZWA kuwa, KMC ikiwa kwenye harakati zake kujiandaa na msimu wa 2021/22, imefanikiwa kuipata saini ya kiungo wa Azam FC, Awesu Ally Awesu.


Kiungo huyo ambaye 
msimu uliopita alikuwa miongoni mwa nyota walioifanya Azam kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ametua KMC kwa mkopo wa mwaka mmoja.

 

Taarifa zilizoifikia Spoti Xtra, zinaeleza kwamba, kiungo huyo hivi sasa yupo Morogoro na kikosi cha KMC ambapo timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na msimu wa 2021/22.

 

“Msimu uliopita Awesu hakupata nafasi kubwa ya kucheza akiwa Azam, mechi alizocheza kwenye ligi hazifiki hata tano, sana sana amecheza katika Kombe la Kagame.

 

“Japo uongozi wa KMC FC haujaamua kuweka wazi ila Awesu yupo Morogoro kambini pamoja na wenzake wakijiandaa na msimu ujao wa 2021/2022,” kilisema chanzo.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa hizo ni tetesi na wakikamilisha kila kitu wataweka wazi kuhusu usajili.


Hivi karibuni, Awesu alisema: “Bado nina mkataba wa miaka mitatu na Azam FC, kutokana na changamoto ya namba ambayo nimekutana nayo tayari nimewasiliana na uongozi kuona uwezekano wa kutolewa kwa mkopo kwenda timu nyingine ili niweze kupata muda mwingi wa kucheza.

 

“Ushindani wa namba kwenye kikosi cha Azam ni mkubwa, hivyo ni lazima upambane ili uweze kupata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic