YUSUSPH Mhilu, ingizo jipya ndani ya Simba akitokea Klabu ya Kagera Sugar amesema kuwa atawashangaza wengi ambao hawampi nafasi ya kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho.
Nyota huyo usajili wake umezua gumzo hasa kutokana na vichwa ambavyo anakwenda kukutana navyo kwenye nafasi ya ushambuliaji ikiwa ni pamoja na nahodha John Bocco kinara wa mabao akiwa nayo 16, Chris Mugalu mwenye mabao 15 na Meddie Kagere aliyetupia mabao 13.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mhilu aliyetupia mabao 9 ndani ya ligi akiwa ni namba moja kwa nyota wa Kagera Sugar wenye mabao mengi alisema kuwa hana mashaka na uwezo wake.
“Nadhani kuna watu wana mashaka kuhusu uwezo wangu hilo ninapenda kuwatoa hofu kwani ninajiamini na nipo vizuri. Tayari nimekomaa na nipo tayari kucheza kwenye timu kubwa.
“Muda ambao nilicheza kwenye timu nilizokuwa ikiwa ni pamoja na Ndanda,Kagera Sugar na Yanga vimenifanya niwe imara na ninaweza kucheza popote ikiwa ni pamoja na Simba ambapo nipo kwa sasa,” alisema Mhilu.
Nyota huyo amepewa dili la miiaka miatatu anakuwa ni nyota wa pili kutambulishwa akiungana na Peter Banda ambaye alikuwa wa kwanza kutambulishwa.







Asitishike mimi ni miongoni mwa watu nnaoamini Muhilu Kama ataepukana na majeraha basi hawezi kukaa Simba miaka mitatu atanyakuliwa kwenye Klabu kubwa Zaidi ndani au nje ya Tanzania. Huyu ndie Cristian Ronaldo wa Bongo asibweteka anaweza kuwa yeye mwenyewe anataka awe ana kila kitu kinachohitajika kuwa miongoni mwa deadly striker watu wanaweza kubeza ila akiamua kujitesa kwenye mazoezi ya ziada hasa yale ya Gym basi tusubiri kuona Mzawa akiwaburuza wageni kunako kutupia kwani nnaimani Muhilu Bora kuliko prince Dube hasa kunako fitness. Ajue tu katika umri Wake sio umri wa starehe hata kama pesa anazopata zinauwezo wa kumpa Starehe. Ni umri wa Kazi zaidi na ni vizuri kuwa na lengo kubwa Zaidi sio zambi. Kwa bahati nzuri Simba Sasa imekuwa ikitupiwa macho mno na timu nyingi za nje kiasi Cha kupandisha thamani wachezaji kutoka Tanzania lazima tuwape hongera simba kwa hilo mtu akubali asikubali huo ndio ukweli.
ReplyDelete