CLATOUS Chama nyota wa Simba leo ameaga rasmi kwa mashabiki pamoja na viongozi wa Simba kwa kumaliza na neno moja kwamba, 'Asanteni Sana'.
Ni rasmi kwamba kiungo huyo mshambuliaji kipenzi cha mashabiki na chaguo la kwanza la makocha wote waliopita ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na Patrcik Aussems, Sven Vandenbroeck na hata huyu wa sasa Didier Gomes hatakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.
Akiwa na miaka 30 anakwenda kupata changamoto mpya na habari zinaeleza kwamba anakwenda RS Berkane ya Morocco na kila kitu kimekamilika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chama amesema:-"Nimekuwa kimya kwa muda tangu mara ya mwisho nitume ujumbe wowote kwenye kurasa zangu za kijamii, ilibidi iwe hivyo kwa sababu kuna mambo nilikuwa ninakamilisha na nilikuwa nasubiri taratibu zote zikamilike. Siwezi kuwaacha nyinyi kwenye giza.
"Stori yangu ilianza pale nilipokuja Tanzania 2018, sikuwa najua kwamba ningeweza kuwapata watu wengi, kuweza kuongea kiswahili lakini upendo ambao nimeweza kuupata hapa hauelezeki katika maisha yangu.
"Siwezi kueleza namna ninavyohisi kuhusu Simba, kwa maneno machache ni kwamba bado ni ngumu kuamini kwamba jina langu halitatajwa na Baraka Mpenja msimu ujao ama sitavaa jezi yangu namba 17 katika timu ambayo ilikuwa ni ya nyumbani.
"Asante kwa viongozi wa Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mr Mo Dewji, CEO, Barbara Gonzalez, uongozi wa timu kiujumla, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzagu pendwa asanteni kwa upendo wenu.
"Kwa mashabiki nitazidi kuwakumbuka nasema asante sana nitazidi kuwasiliana nanyi kupitia mitandao ya kijamii, nitaendelea kushangilia pamoja nanyi labda ikitokea nikacheza nanyi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa heri na asanteni" .
"Asanteni Sana'.
Unatuumidha thithi lkn tunatamani kujiua,tumekata tamaa mie naamia PSG kukwepa kutanzi nimekata tamaa ya soka la Bongo ,maana Utopolo wamekuja kivingine ,tumesajili watu Saba kudhiba nafasi yako na Louis lkn bado hatujawa na uhakika.Ee mola tuepushie hili balaha
ReplyDeleteYou were the player to watch, you kept the ball rolling, you kept the team playing and believing in winning. Do you remember your goals against AS VITA and Nkana. The goals to remember.
ReplyDeleteThe best player recent centuries in our club.
Thank you SSC for a such a talented and hard worker player.
Otherwise, I wish you, CCC, the rock of Lusaka all the Best. Asante sana na wewe!
English au siyo🤣
DeleteInakupa shida sana? Hapa ndo pakujifunza . Andika unachoeeza, zungumza unachoweza. Nikukumbushe tu, kingereza ni lugha kama lugha zingine. Tofauti yake ni umaarufu tu
DeleteKakimbia FDL au Champions League kwa jina jipya la hapa Bongo. Tarehe 24 inakaribia CAS hoyeee!
ReplyDeleteWabongo Bwana mwenzio anasema anatamani angekuwa hapa anajifunza Kiswahili ,wewe huku post Kiingereza kwani na Hilo goal na Nkana tutalipenda cse lilikuwa la ushindi/kutupitisha lkn ndiyo ule Mpira tunaita vanga vanga,Mimi nakumbuka yule Refa Mkenya siku hiyo simtofautishi na yule mapunda mliyosema alikuwa anahamasisha
ReplyDeleteNi kweli unachosema, lakini na mimi napenda kukifunza kingereza kama yeye anvyolenda kukifunza kiswahili. Kwa taarifa yako lile hili la Nkana lilituvusha kwenda kwenye makundi.
DeleteEng Kyando, utaumiza kichwa chako kubishana na watu ambao hujui wameamkia chaka gani na pengine wameamkia kwenye vilabu vya matapu-tapu.Ukitaka kujua huyu Mwamba wa Lusaka, triple C, rejea magoli yake ktk video clips dhidi ya Nkana, AS vita na hata yale dhidi ya Kaiser Chiefs, Plateau na Biashara United ndio utajua kwa nini Baraka Mpenja alisema unaona kama mimi ??
DeleteHivi umemuelewa Chama kuhusu....'hakujua angepata watu wengi hapa Tanzania na kuongea kiswahili'na sio wewe unavyotafisiri 'kuwa angetamani kuwa hapa na kujifunza kiswahili'...Wakati amekaa Tanzania takribani miaka mitatu na ameondoka akijua kuzungumza kiswahili.Usikurupuke kukosoa wenzako wakati wewe mwenyewe huelewi unachokosoa.
DeleteCHAMA KWAMBA KIMBIA HAWAJAJA WAHI MPE BOKO LKN MUNGU AKASAIDIA BOKO AKAPIGA KIDUCHU/KIJISHUTI.Namaanisha game ya Simba vs Yanga tarehe3/7/2021.
ReplyDeleteNo player is irreplaceable, kwakheri triple C, karibu Sakho, Banda, maisha yaendelee
ReplyDelete