ISRAEL Mwenda, beki wa kulia kutoka Klabu ya KMC kwa sasa ni mali ya Simba baada ya kutambulishwa rasmi leo Agosti 16.
Nyota huyo alikuwa nahodha katika timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 iliyotwaa taji la Cecafa Challenge 2021 nchini Ethiopia.
Akizungumza baada ya kutambulishwa leo beki huyo amesema kuwa atapambana kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo.
"Nitapambana kwa ajili ya kuipa mafanikio timu yangu kwa kuipa mataji pamoja na ushindi kwa kuwa malengo ni kuona kwamba tunafikia malengo.
"Kila ambapo ninapata nafasi nimekuwa nikipambana ili kufanya vizuri hivyo kwa kuwa nipo kwenye changamoto mpya basi nitashirikiana na wengine, ".
Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22. Nyota huyo inatajwa kuwa amesaini dili la miaka miwili.
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Septemba 29 na Septemba 25 mchezo wa ngao ya Jamii unatarajiwa kuchezwa.
Mnyama akipenda Mungu wetu kwa miaka mingi ijayo ataendelea kunguruma na kati ya timu bora Africa
ReplyDeleteDogo nenda kasugue benchi akili ikukae sawa,muulize Ilanfya aliishia kukaa jukwaani
ReplyDeleteMikia ni hatari, wagumu sana kuwapa nafasi madogo kwani wakifungwa hata mechi ya kirafiki kelele zake hapata kalika.
ReplyDeleteKarb mwenda kwenye timu yamakombe
ReplyDeleteTusiwakatishe tamaa na kuwatisha vijana kwa roho mbaya ya kishabiki. Tuwape moyo ni kizazi kipya lazima tuwajenge katika kujiamini.
ReplyDeleteNa Sina uhakika ila Jina la Mwenda asili yake Morogoro na asili ya watu wa Morogoro ni wapambanaji sio legelege na ukimuona legelege basi ni feki huyo na Kama hivyo mwenda nenda kapambane ziba masikio usije ukageuka jiwe,show me(shomi) will show you the way.
Aende akakae bench huyo mpaka alie kama mbaga
ReplyDeleteUtopolo hamna timu?Kazi ku comment timu ya wanaume.
ReplyDelete