August 20, 2021


RASMI leo Agosti imemtambulisha kiungo aliyekuwa anakipiga ndani ya Al Ahly Benghazi ya Libya, Sadio Kanoute mwenye umri wa miaka 24 kuwa mali mpya ya kikosi hicho.


Anajiunga na mabingwa watetezi ambao wameweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dau ambalo anatajwa kupewa nyota huyo ni zaidi ya milioni 300 kwa ajili ya usajili wake na ni dili la miaka mitati ambayo anatajwa kusaini.


Ni kiungo mwenye uwezo wa kukaba na kushambulia ikiwa atapewa nafasi na uwezo wake ukajibu ndani ya Simba inayonolewa na Didier Gomes.


Kiungo huyo amesema kuwa ni furaha kwake kujiunga na Simba hivyo atafanya juhudi kutimiza majukumu yake.

12 COMMENTS:

  1. Huu usajili nilikuwa nausibiri kwa hamu. Safi sana. Lakini mbona idadi imezidi?

    ReplyDelete
  2. Idadi haija zidi acha kiherehere kwani simba ilisha tangaza kikosi rasmi Cha msimu ujao? ila hili Jembe we acha tu ataufamya ujembe wa Saleh Jembe uonekane feki mwaka huu��

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wee jamaa nimecheka na jinsi ulivyomjibu jamaa hapo ety wamezidi

      Delete
  3. Ila hii picha vipi? Anatambulishwa mchezaji wa Simba au Alhaly bengaz?

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo kuna watakaoachwa au kupelekwa loa au watasajiliwa michuano ya CAF tuu kama ilivyokuwa kwa kahata last year.

    ReplyDelete
  5. Nahisi chikwende na kagere watapisha nafasi, maoni yangu tuu

    ReplyDelete
  6. Yanga wanapata tabu sana.

    ReplyDelete
  7. Wanasema eti wanajibu mapigo ha ha ha ha ha nawaonea huruma sana.acha tusubiri muda.

    ReplyDelete
  8. Wamejibu, wamemtambulusha bangala litombo, yanga sasa ina wakongo 6

    ReplyDelete
  9. Shida Ni kwamba mna Wachezaji 13 ,lkn Mzee wa ung'eng'e hata Chikwende alimpamba ,Ila mmejitahidi kuziba nafasi ya Chama na Louis Wachezaji Saba mpaka Sasa,kweli Wazee wa Kikosi Kipana,hao Aly Ahyl mpaka Sasa wamepeleka CAF Wachezaji 33,lkn naomba niulize kile kitasa Cha Zimbabwe Kiko wapi?

    ReplyDelete
  10. Hongera simba sc kwa usajili wa huyu mwamba kaz iendelee

    ReplyDelete
  11. Kikosi cha Yanga kutakuwa cha wakongomani tu. Wakiamua kuihujumu timu ni rahisi sana. Yanga inatakiwa waliangalie sana hili suala. Walipaswa kuchanganya raia tofauti tofauti ili kuleta ufanisi kwenye Kikosi Chao. Kila la kheri timu ya Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic