WAMEJIBU ghafla mabosi wa Yanga baada ya muda mfupi watani zao wa jadi kumtambulishwa Sadio Kanoute hawajapoa kwa kuwa wameachia nao mashine ya kazi.
Anaitwa Yanick Bangala Litombo ambaye ametambulishwa leo rasmi kupitia ukurasa rasmi wa Yanga kwa maneno mafupi kwamba, "Bangala is Green and Yellow') (Bangala ni kijani na njano).
Kwa sasa Yanga wapo zao nchini Morocco ambapo wameweka kambi ya muda wa siku 10 na huyu mchezaji wao wa leo anakuwa wa 11 kutambulishwa baada ya wale wengine Wacongo waliotambulishwa ikiwa ni pamoja na Heritier Makambo, Fiston Mayele na Djuma Shaban.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa amebainisha kwamba wachezaji wote ambao wamesajiliwa pamoja na mipango kazi itazinduliwa rasmi Agosti 29.
Siku hiyo itakuwa ni siku ya kilele cha Mwananchi hivyo majembe yote ya kazi ikiwa ni pamoja na mzawa Dickson Ambundo naye atatambulishwa pia.
Inatajwa kuwa dili ambalo amesaini ni miaka miwili kwa ajili ya msimu wa 2021/22.
Tumejibu mapigo ha ha ha ha raha sana.
ReplyDeleteSasa first eleven ya yanga itakuwa na wacongo 6
ReplyDeleteSio mbaya,chamsingi jiandae kisaikolojia,mtakufa ndani nje,tukianza na ngao ya jamii.
DeleteMbona Azam ilikuwa na waghana 6, kisha wazimbabwe 6 na hamkusema kitu?
DeleteSawa
ReplyDeleteKasuka kama joketi
ReplyDeleteKama mama ako fara wew
DeleteTwende twende congo fc
ReplyDeleteWakimbizi fc
DeleteMakocha watatu watoweka yanga.
ReplyDeleteDaima mbele nyuma tuwaachie mikia fc...
ReplyDelete