SASA ni rasmi Cristiano Ronaldo raia wa Ureno msimu wa 2021/22 ni mali ya Manchester United baada ya mabosi wa timu hiyo kumtambulisha rasmi kwa kusema kwamba yupo nyumbani.
Taarifa rasmi iliyotolewa katika Ukurasa wa Instagram wa Manchester United uliandika maneno mafupi kwamba Cristiano yupo nyumbani na kusindika na picha ya Cristiano Ronaldo katika mapozi tofauti.
Gumzo kubwa katika usajili wa Ulaya awali lilikuwa kwa Harry Kane wa Tottenham pamoja na Jack Grealish aliyekuwa anakipiga ndani ya Aston Villa ila kwa sasa ni mali ya City kabla ya United kutibua dili la Ronaldo kujiunga na City akitokea Klabu ya Juventus.
Ni dili la miaka miwili amesaini Ronaldo ndani ya Manchester United ambapo anarudi hapo baada ya miaka 12 kupita na alipokuwa hapo alifunga jumla ya mabao 118 katika mechi 292 alizocheza kati ya mwaka 2003 na 2009 alitwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya na FA Cup pia alitwaa mataji mawili ya League Cup.
Anakwenda kuwa chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer ambaye aliwahi kucheza naye ndani ya United huku akibainisha kwamba ni ngumu kumuelezea Cristiano.
Congratulations for everyone, no life without football
ReplyDelete