August 26, 2021

 


MAHAKAMA ya usuluhishi ya masuala ya kimichezo CAS bado haijaweza kutoa maamuzi yoyote yale kuhusu kesi ya mchezaji wa Simba kwa sasa Bernard Morrison maarufu kama mzee wa kuchetua.

Bado ngoma ni mbichi kwa kuwa muda wowote ule hukumu hiyo inaweza kutolewa.

Kwa mujibu wa CAS kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu siku ya Agosti 24 ila mpaka kufikia majira ya saa sita usiku ngoma ilikuwa haijaeleweka bado.


Klabu ya Yanga ilipeleka shauri lake kwenye mahakama hiyo wakimlalamikia Morrison kuweza kusaini dili jipya ndani a Simba ilihali alikuwa na mkataba wa miaka miwili ndani ya kikosi hicho.


Kwa upande wa mchezaji mwenyewe alikuwa anabainisha kwamba alisaini dili la miezi sita ndani ya Yanga na muda wake uliisha hivyo alisaini dili jipya akiwa ni mchezaji huru.


Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema kuwa nao pia walikuwa wanasubiri majibu kutoka Cas ila hawakuyapata jambo ambalo linawafanya waendelee kusubiri.


"Matarajio yetu ilikuwa ni kuona kwamba tunapata mrejesho wa kesi kwa kuwa hayajatoka basi ni suala la kusubiri kwa kuwa kesi kuna taratibu zake za majibu kutoka," .

7 COMMENTS:

  1. Kwa Morrison Yanga wameteseka na wataendelea kuteseka Sana.

    ReplyDelete
  2. CAS yenyewe vimeo, taasisi timamu inaheshimu deadline, kwann mpaka imevuka tarehe waliojiwekea hakuna mrejeshi? Uzembe hauko Africa peke yake, dinia nzima kuna wazembe

    ReplyDelete
  3. Taarifa tunazo yanga wamepoteza point kwenye ishu hiyo kamwe yanga hawezi kushinda walifoji sahihi nashangaa taasisi kubwa kama yanga inaghushi sahihi ya mchezaji jambo ambalo litawaweka sehemu mbaya haya ndiyo Yale ya simba na sindano na ndiyo maana wamemchukua manara ili kuzima kelele za washabiki wao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hiyo CAS wamewapa Yanga majibu kwa siri au

      Delete
  4. Kabisa viongozi wa Yanga tayari wanazo taarifa za kushindwa kwenye kesi ya Morrison. Wanahangaika jinsi ya kutuliza mashabiki wao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa ufahamu wangu hukumu ingekuwa inetolewa, lazima upande wa Mshtakiwa pia ungekuwa na taarifa.
      Naamini haijatoka hukumu bado, na haitakuwa siri kwakuwa kuna pande 2 tofauti ambazo zitapata hukumu hiyo na kwa mbwembwe za Morson lazima angepost ushindi.

      Delete
  5. Mwenye Taarifa sahihi za hukumu hiyo atupe tuone Tusilete Ushabiki ili tujue Nani Mkosaji CAF au Yanga!?!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic