August 26, 2021

 


GEORGE Lwandamina,  Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wanafanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika mchezo wa kirafiki dhidi Red Arrows. 


Kwenye mchezo huo wa kurejesha utimamu wa mwili Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 huku Lwandamina akiweka wazi kuwa kuna jambo ameliona kwa wachezaji wake.


"Nilikuwa nataka kuona wachezaji wanarejea katika utimamu wa mwili hasa kutokana na uchovu pamoja na kukaa muda mrefu bila kucheza mechi za ushindani.


"Hata namna wachezaji walicheza bado walionekana hawajawa tayari hivyo taratibu wanarejea katika hali ya kawaida ni jambo la kusubiri," amesema. 


Azam FC imeweka kambi nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 na itawakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ikiwa ipo kwenye Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic