August 27, 2021


 BAADA ya mastaa wengine wa kikosi cha Simba kusepa Morocco kutokana na majina yao kutajwa kwenye timu zao za taifa, kocha wa viungo wa Simba Adel Zraine amewakomalia mastaa wa Simba waliobaki ikiwa ni pamoja na Chris Mugalu, Bernard Morrison na Rarry Bwalya.

Kocha huyo wa viungo amekuwa akiwasimamia vijana hao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wachezaji ambao wameitwa timu zao za taifa wana kazi ya kutimiza majukumu yao walikoitwa huku wao wakiendelea na wale waliobaki.

“Kwa wachezaji ambao wameitwa timu zao za taifa lazima waendelee na majukumu yao huko walikoitwa nasi tutaendelea kubaki na wale ambao wamebaki kambini kikubwa ni kwa ajili ya maandalizi.

“Kiujumla maandalizi yanakwenda vizuri na kila kitu kinakwenda sawa,” alisema Rweyemamu.

Kikosi cha Simba kurejea Tanzania wiki hii kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea katika Simba Day inayotarajiwa pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Septemba 25.

2 COMMENTS:

  1. Ni kweli kazi inaendelea. Mashujaa wamecheza na timu isiyofungika bila ya kuogopa matokeo na huku mlinda mlango akiwa mmoja tu hakuna wa akiba tena kipa namba tatu wa timu anbaye hakuwa akipata nafasi na katika kikosi, hawakuogopa wala kufikiria vipi pindi kipa huyo angepata majeraha au kutolewa kwa kadi nyekundu nani badili angekuwa. Juu ya hayo yote waliondoka na droo na kuumiliki mpira kuliko wenyeji. Hiyo ndio tabia ya Simba asiyeogopa au kukata tamas

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic