August 27, 2021


 KUELEKEA kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Agosti 29, Haji Manara ameweka wazi watafunika zaidi ya ile ya mwaka 2020 na ameweka wazi kwamba wao tamasaha lao lilibuma mwaka jana.

Manara ameibuka ndani ya Yanga akitokea Simba ambapo aliweza kuhamasisha mashabiki wa timu hiyo kuweza kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Simba Day ila kwa wakati huu anahamasisha watu wajitokeze Mwananchi Day.

Tamasha hilo kwa sasa linaendelea ambapo mashabiki Tanzania wamekuwa wakiendelea kutoa misaada kwa jamii na kutoa damu pamoja na kufanya usafi huku kilele kikitarajiwa kuwa Agosti 29, Uwanja wa Mkapa na utapigwa mchezo wa kirafiki.


Manara amesema:"Sisi tamasha letu lilidoda mwaka jana tulipigwa bao na Yanga ila kwa ubishi wangu na kujitutumia ikaonekana kama tuko sawa, sasa kwa sasa nikiwa nimekuja huku unadhani nini kitatokea?

"Yanga wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa jambo ambalo limenifanya nije huku sasa. Tulifunga screen pale uwanja wa jirani ila zilidoda waliingia watu 20 tu tofauti na wenzetu," .

12 COMMENTS:

  1. Karibu nyumbani kumenoga, tutakupa ushirikiano mkubwa, karibu sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Manara anajikuta anaisemea Simba bila kujijua.Simba wameshapita kwenye matamasha kama mtaji.Simba ni kampuni rasmi Sasa mvua inyeshe au isinyese mishahara ya wachezaji na huduma nyengine zipo kwenye pay roll.Vigumu kuwekera Simba huku wakiendelea kubeba mataji. Yanga kujifariji kwa porojo za Manara ni dalili ya kukata tamaa kwenye mbio za ubingwa.Manara yeye hata apige dana dana uchi kwa simba hii atajidhalilisha mwenyewe.Manara anakwenda kuwaponza Yanga kwenye historia mbaya wasioitarajia,Amen.

      Delete
  2. Kwan yanga waliingia viwanja vi2 au ki1??? Sawa manara,, kaza kaza! Majibu yatapatkana punde ipi timu kubwa

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa atachizika bure kwa kufikiria simba, atakuwa anaumia sana kufurumishwa. Pambana na hiyo mme mpya ndio maana ya kuachika ja kuolewa pengine.

    ReplyDelete
  4. Manara amesema:"Sisi tamasha letu lilidoda mwaka jana tulipigwa bao na Yanga ila kwa ubishi wangu na kujitutumia ikaonekana kama tuko sawa,

    Kumbe Manara bado yupo Simba!!!! Tafakari kauli yake hiyo

    ReplyDelete
  5. Mke ukimuacha halafu ukaona kila kukicha haishi kukusema ujue kaumia sana

    ReplyDelete
  6. Sasa na ninyi si mkae kimya ?au mna missiana tuelezeni Mikia

    ReplyDelete
  7. Kuna sehemu mpaka mtu abaitwa kigogo naye kawaka ,kisa Haji

    ReplyDelete
  8. Ahahahaha! Hureeeee aisee litakufa jitu mwaka huu

    ReplyDelete
  9. Ameondoka Simba anasema sisi tamasha lilidoda badala ya kipindi nipo Simba yanga ilifunika Simba,sijamuelewa au ana usimba bado ameondoka na sisi Simba asiitumie Bali sisi yanga ndo atakuwa kasepa kweli

    ReplyDelete
  10. Wanajangwan wenzang kwa maon yangu mm haji manara amekuja ku2vuluga maana kauli zake hata hazieleweki

    ReplyDelete
  11. Utopolo wameingia chakike, wanaume funapambana kwaajili ya nda I na kimataigz kuhatetea makombe yetu Hawa uto wanaimba taarabi baadae waanze kuwalaumu marefa na TFF hoo tunaonewa n.k

    Mpira sayansi siyo porojo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic