DUNIA imewahi kushuhudia watu
wengi maarufu waliopata kuibukia katika taaluma mbalimbali. Katika ulimwengu wa
Sayansi na Teknolojia mwaka 1879 alizaliwa mtu mmoja maarufu aitwaye Albert
Einstein.
Einstein amekuwa maarufu sana
hata baada ya kifo chake kilichotokea mwaka 1955, hii ni kutokana na kuwahi
kufanya mambo mengi yaliyowashangaza watu. Kuna wakati mtu huyu maarufu aliwahi
kusema “Wendawazimu ni kufanya kitu kilekile kila wakati, huku ukitegemea
matokeo tofauti.”
Bila shaka unaweza kujiuliza ni
kwanini nimeanza na stori hii? Subiri nitakuelewesha, kwa sasa kwenye Ulimwengu
wa soka maeneo mbalimbali, ligi zimeshamaliza na kinachoendelea ni maandalizi
ya kabla ya msimu ‘Pre-season’, pamoja na masuala ya usajili ambayo ndiyo
habari ya mjini.
Kwetu hapa Tanzania
unapozungumzia usajili basi huwezi kuacha kuzitaja klabu za Simba, Yanga na
Azam ambazo mara zote zimekuwa zikivuta hisia za wadau wengi wa soka.
Kama ilivyokuwa msimu uliopita,
msimu huu pia Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara klabu ya Yanga, wameteka
stori za usajili kutokana na kushusha majembe yenye majina makubwa kuelekea
msimu ujao.
Mpaka sasa Yanga wametambulisha
mastaa watano wapya ambapo wanne kati ya hao ni wachezaji wa Kimataifa ambao
ni; Fiston Mayele, Heritier Makambo, Khalid Aucho, Djigui Diarra na
mshambuliaji mzawa Rajab Athuman.
Yanga pia wametangaza kuachana
rasmi na makipa wao wawili Faroukh Shikalo na Metacha Mnata, huku wakijiandaa
kutangaza kuachana na nyota wengine zaidi ya watano wa kimataifa.
Ukumbuke pia katika hili wapo
nyota wengi wazawa ambao wanatarajiwa kupewa mkono wa kwaheri, kutokana na
kushindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa.
Kitu wanachokifanya Yanga kwa
sasa ni kama marudio ya kile ambacho kilifanyika msimu uliopita, ambapo Yanga
waliachana na rundo la mastaa ambao kwa idadi walikuwa wanafika wachezaji 17.
Umegundua kitu? Kama hujagundua
basi hapa ndipo tunaporejea maneno ya Mwanasayansi, Einstein kuhusiana na
tafsiri ya Uwendawazimu.
Kuna kitu hakipo sawa kwenye
Kamati ya usajili ya Yanga, haiwezekani kwa misimu miwili tu waachane na zaidi
ya wachezaji 17, ambao hawakumaliza mikataba yao, kutokana na kushindwa
kuthibitisha ubora wao.
Yanga kwa matumaini makubwa
waliuanza msimu uliopita wa 2020/21, hii ni baada ya kuwa na safari nyingi za
kwenda pale Terminal 3 ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa
lengo moja kubwa la kuwapokea wachezaji wao wapya.
Baadhi ya mashabiki hawa
walidiriki hata kukubali kutengeneza mistari kama vile Wanajeshi wanaojiandaa
na Gwaride, ili wachezaji hao wapya wapite.
Mwezi Agosti ulipoisha na kelele
za mapokezi ya wachezaji kusahaulika, mwezi Septemba ukafika na Ligi ikaanza,
hapo ndipo kasheshe ikaanza kwani mchezo wa kwanza tu Yanga wakatoa sare kwenye
dimba la Benjamin Mkapa dhidi ya Tanzania Prisons, Wananchi wakajipa moyo kuwa
kuteleza si kuanguka.
Baada ya hapo Yanga wakacheza
michezo mitatu, ya ushindi ambao kwa jicho la tatu ulikuwa haupendezi kwani
timu ilikuwa ikicheza bila kuwa na plani inayoeleweka na kuonekana wazi
wamekosa muunganiko, hivyo kusababisha malalamiko kuanza.
Mchezo wa tano tu ukatosha
kumfungulia njia ya kutokea kocha Mserbia, Zlatko Krimpotic na nafasi yake
kuchukuliwa na Cedric Kaze. Kaze akaibadilisha Yanga na kurudisha muunganiko wa
kitimu licha ya kupata shida kupata matokeo ya ushindi.
Kaze akaipa Yanga kombe la
Mapinduzi tena kwa kuwafunga Simba kwenye fainali januari 13, mwaka huu, huku
akipoteza mchezo mmoja pekee, lakini ushindi mmoja katika michezo sita
iliyopita kumewaibua viongozi wa Yanga na kuamua kuwaondoa.
Lakini unaweza kujiuliza tatizo
la Yanga liko wapi? Ni kweli kulikuwa na shida ya benchi la ufundi? Au shida
ipo kwa madaraja ya wachezaji walionao? Na vipi kuhusu uthabiti wa Uongozi?
Bila shaka hapa ndipo tunabaki na
swali gumu zaidi, juu uthabiti wa mbinu za usajili zinazotumiwa na Yanga kuleta
wachezaji wapya, bila shaka ligi itakapoanza Yanga itakuwa na deni kubwa la
kutuonyesha utofauti wa kilichofanyika kwenye usajili wa mwaka jana na wa mwaka
huu.
Ikiwa watarudia makosa yaleyale basi sisi tutarudi kwa Mwanasayansi, Einstein na tafsiri yake ya Wendawazimu.
Uchambuzi wa Vuvuzela kwenye gazeti la Championi Jumatano
Sisi yanga tunataka simba tu iwe timu kubwa wote hamieni huko na muendelee kutumika sisi na yanga yetu tunasonga mbele ndio maana munawasifu washambuliaji hatari mechi 34 magoli 16 tupeni wastani kila mechi kafunga magoli mangapi
ReplyDeleteKuwa makini: Hakuna striker Simba aliyecheza mechi 34. Pia mfungaji bora anapatikana kwa idadi ya magoli sio wastani
DeleteTatizo la Yanga ni mikia kuamua kununua bidhaa dukani kwa Yanga
DeleteHospital inakuhusu we mwandishi mana unacho zungumza ni kma umekula mavi tu
ReplyDeleteMWENDA WAZIMU NI WEWE MWANDISHI UNAE TESEKA KWA KUONA YANGA IMEFANYA USAJILI MZURI AMBAO UNA TISHIA MAFANIKIO YA SIMBA KWA MSIMU UJAO. KAMA UNATESEKA SANA JIUE TU, ILI MATESO YASIENDELEE.
ReplyDeleteLigi haijaanza unasema unatishia mafanikio ya Simba, unajua timu yako ifapafom vipi? Sifa za kwenye vyombo vya habari zimekuaminisha kitu ambacho ujalilisia wake bado haujaonekana matokeo yake mnaishia kulalamika kila uchwao
DeleteUjalilisia___ uhalisia
DeleteMwandishi kama huyu ni kama chizi alokula kinyesi chake kwa sababu jana yake alikula pilau, ndo maana manara aliwaita takataka
ReplyDeleteWewe Mwenye akili kawasaidie Simba waombe waongezwe Wachezaji 12 maana vi,le Vimeo haviuzwi popote ,msimu iliyopita tulitumia Sana wazawa foreinger wengi wali fell Sasa tunajaza nafasi ikiwa na kuondoa Maduka unapansisha Acid,Wambie Simba aliyewafanya wawape mikataba akina Chikwende wajilaumu kwa ndani tunajaza it's only 10 tu,
ReplyDeleteSimba wanaingiaje hapa au ndo kuweweseka. Tumia hoja kupinga jina jipya hilo alilowapa mwandishi. Simba haihusiki hapo
DeleteAmkeni amkeni, kumekucha huku wamepewa jina lingine buana. Wanaitwa WENDAWAZIMU
ReplyDeleteUkuma ni nini, ni pele unapojifanya unajua kuchambua mpira wakati mwenyewe ni kondom, mwandishi ww ni kuma, ni kisimi na we ni mavi
ReplyDeleteMatusi ya nini sasa Kama huna hoja za msingi si ukae kimya
DeleteKuna watu fulani humu wanapenda sana kutukana kumbe tumeshajua ukiona mtu anatukana humu ujue huyo ni MWENDAWAZIMU
ReplyDeleteSaleh Jembe hana akili
DeleteTatizo la mashabiki wa Yanga wengi ni makanjanja , Hata hawasomi na kuelewa Mwandishi amemaanisha nini , Wanakurupuka na kuanza kutukana, Usajili wa Yanga ni mbovu sana na Lazima wakubali na kuitathimini, Ni kweli kwamba wachezaji wa kimataifa wa Msimu uliyopita wazuri ni wawili tu ? kama ni hivo injinia hafai kuwa kwenye kamati ya usajili au ni mpigaji ! Anatumia brand ya Yanga vibaya kwa maslahi yake binafsi ! Yanga wanasajili nusu ya kikosi kila msimu ? ! Inashangaza sana
ReplyDeleteUmeandika upuuzi
Deletemfano au kauli ya mwandishi imelenga kutusi zaidi,imetoka kwa mtu asie na upeo wa soka ,mfano mdogo,unaandika.haiwezekani kwa misimu miwili tu waachane na zaidi ya wachezaji 17, ambao hawakumaliza mikataba yao, kutokana na kushindwa KUTHIBITISHA WAO.dunia nzima mchezaji huachwa kwa sababu hiyo kushindwa kuthibitisha UBORA.simba hii unayoiona imepita ktk kipindi kama hiko.ndio lamine,wale wazaire,na wengine wengi,halafu kwenye soka sio kama maabara ya sayansi kwamba unachanganya chumvi na limao wakati wote ukitegemea kupata ladha tofauti,kwenye soka,mukoko sio bigirimana.wala kisinda sio ngasa,aliwahi kusema josse mourinho anahitaji madirisha matatu ya usajili ili kupata timu.kufanya vizuri ni jambo jengine,mfano makipa,wakati timu inatafuta nafasi ktk mechi za mwisho,kipa anaruka kudaka huku kakunja mikono washabiki wanalalamika anawatukana,huyu mwingine ni mzuri ila hatoshi,yanga na azam mwisho wa mechi unaona kipa angekua bora zaidi asingefungwa.mwingine anaweza ruka peke yake akadaka mpira bila kugusana na mtu akauachia mtu akaja akafunga.hiyo dodoma jiji al ahly.kwa hiyo mabadiliko ni ya lazima.na hayafani.hivi ni vipindi vya mpito kote duniani nyakati flani hutokea,hivyo mpira na hiyo kauli ya mwanasayansi,haviendani nikutaka kutukana watu,ama upeo mdogo.
ReplyDeleteSaleh Jembe WEWE AKILI YAKO HAINA AKILI
ReplyDeleteMatusi ya nini?Hoja hujibiwa kwa hoja.Ukiona unaanza matusi ujue huna hoja.Mpuuzi ni yule anayekimbilia kutukana.
ReplyDeleteDuu watu wana matusi mpaka sio vizuri
ReplyDelete