ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amethibitisha kuwa kuna uwezekano mkubwa akaifungulia mashitaka klabu ya Yanga kwa Shirikisho la soka la Kimataifa FIFA, kuhusiana na madai ya stahiki zake.
Inaelezwa kuwa kocha huyo anawadai Yanga kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 115 za Kitanzania.
Pluim, aliiongoza Yanga kama kocha mkuu kwa vipindi viwili tofauti kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, huku pia akiwahi kushika nyazifa nyingine ndani ya klabu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema: “Taarifa za mimi kuwa kwenye mpango wa kuwapeleka Yanga FIFA ni za kweli, lakini nisingependa kuzungumza sana kuhusu suala la kesi hii kwa sasa, kwa kuwa kuna wawakilishi wangu ambao wako Dar es Salaam kwa ajili ya kushughulikia kesi hii.”
Tulipomtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Taarifa za kudaiwa na kocha Hans zinapaswa kuwekwa sawa kwa kuwa ni
kweli alikuwa akitudai, lakini tayari suala hili lilishafanyiwa kazi.”
MWANDISHI USIJARIBU KUTUSAHAULISHA KUNA SHAURI LA SIMBA KUHUSU MORISSON KULE CAS NA JUMAMOSI HUKUMU ITATOKA.
ReplyDeleteUsihamishe mada suala la Morrison lilishaandikwa. Kila mara timu inapelekwa FIFA kwa madeni, aisee msipokuwa makini mtatumbukia pabaya
DeletePesa tunazo lakini tumeshazoea vurugu na kugombana. Tunapenda kushtaki na kushtakiwa
ReplyDeleteHuu ni WENDAWAZIMU wa kiwango cha lami
DeleteSishangai hizo ndo akili za kiutopolo
DeleteUtopolo munatutia aibu malizana na mzee akanywee kahawa
ReplyDeleteHuyu Mwandishi anaibua hizi taarifa kuharibu Usajili,kweli Manara kawavuruga Mikia
ReplyDeleteUsajili unavurugikaje sasa hapo, lipeni pesa acheni dhulma itawaletea mikosi
DeleteHivi Dante alishalipwa? Nauliza tu
ReplyDeleteWatalipwa tu,halafu matatizo ya madeni timu zetu zote zinakumbwa nayo,NI muda na season tu tunapishana
ReplyDeleteHakuna kitu Kama hicho lipeni madeni utapeli mbaya MUNGU hapendi mtalaaniwa
DeleteDhulma ndizo zilizowanyima matopolo mbali ubingwa lakini hata Kagame
ReplyDeleteWao fujo tu tena sio vijana tu bali hata waliopindukia umri wa 80
ReplyDelete