August 29, 2021

 


KIKOSI cha Yanga leo kimepoteza katika mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa.

Alianza  Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 lilikuja kusawazishwa kipindi cha pili Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.

Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.

Mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi na licha ya timu yao kupoteza bado waliwashangilia wachezaji wao.

25 COMMENTS:

  1. Niliwaambia nyie ni wacheza mayenu sio soka, ona sasa huyo wakudaka mishale yuko wapi? Punguzeni mdomo nyie, ndo maana mkamchukua manara mkidhani maneno ndo yanaleta ushindi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vipi MANARA aliingia dakika ya ngapi? Naona ndie mchezaji alieimbwa Sana kuipa matokeo chanya Yanga imekuaje tena? Lakini referee alikuwa ni wa simba yule😄🤧😫
      Mwana kulitaka mwana kupakatwa👻

      Delete
  2. Matokeo ya leo ...yanga princes 1-1 Ilala queens, yanga U20 1- 3 Cambiasso sports academy, Yanga Utopolo 1 -2 Zanaco.... Wanachojua ni kucheza mayenu tu

    ReplyDelete
  3. Wako wapi mbona wamejificha wakuye wakuye ulingoni huku

    ReplyDelete
  4. Asante ZANACO kwa kusafisha hali ya hewa maana mtaani Utopolo walikuwa wanasumbua utafikiri game inachezwa mdomoni,mpira ni long term plan,cyo Domo Domo Kama Manara na hapo Bado River United ya Nigeria,mwaka huu hata kombe la mbuzi hampati mtaishia mpira wa mdomoni wakati Wekundu wakitusua kimataifa,nasikia na leo refa kawabeba ZANACO kisa mmenyimwa penalt.Sasa subirini muone mziki wa Simba day

    ReplyDelete
  5. Makorokoro Fc AKA Mikia ,hii Ni pre season na Ni friendly na tumeamua kutafuta Timu ngumu ,hv ninyi hiyo Simba day mnacheza na Nani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Manara kawaingiza Chaka muulizeni vizur Kuna uhusiano gani kati ya Simba na makolokolo muone atajibu nini, jezi za utopolo ndo zina makolokolo. Na bado atawaingiza Chaka Sana huyo

      Delete
    2. Unajitetea kwa hoja dhaifu eti ni preseason na ni friendly mech,kwani simba alicheza na FA Rabat club bingwa?au olympique de ambayo pia ipo ligi kuu ya moroco(batola pro)?kwa sababu gani?fa rabat anacheza shirikisho kama hujui na kwa bara la Afrika ukanda wa waarabu ndio wenye mpira mgumu kuliko ukanda wowote Afrika,simba amejipanga na yupo siriasi sana kwenye maandalizi,zanaco sio wazuri wakulinganisha na fa rabat na ukizingatia mmecheza machinjioni(kwa mkapa) unadhani kama mtu anajielewa utatumia mbinu gani kumbadili asiaminin alichokiona na tayari kimetokea.tengenezeni timu.

      Delete
  6. Wahenga walisema penye ukweli uongo hujitenga,matokeo mechi za Simba Morocco,Simba 2 As far Rabat 2, Simba 1 Olympique 1, nafikiri watu leo wameona uongo na ukweli,Simba kacheza a way na team za kiwango cha juu na zote kapata draw,Kwa Mkapa inajulikana ni machinjio ya team yoyote,muulize As Vita au Al Ahly watakwambia,Sasa nyinyi Utopolo mbele ya fans elfu 60 mmenyukwa,muziki wa Simba mtauweza? Mtaishia maneno ya Haji Manara na mzee Mpili baada ya kuweka strategy kwamba Simba walifanya Nini mpaka preliminary round ya CAF hawachezi,kweli Simba baba lao

    ReplyDelete
  7. Nyota njema huonekana ahsubuhi
    Utopolo tayari Chali Cha mende

    ReplyDelete
  8. Mdau kauliza Simba day tunacheza na Nani? Jibu ni Etoile du sahel,Esprance,Horoya ya Guinea au team ambayo ishawahi kuchukua ubingwa wa CAF,request zimetumwa,tunasubiri taarifa rasmi ya team next week,Ila mkubali au mkatae Simba kwa Tanzania Hana Arch Rival(mpinzani was jadi),Young kutengeneza team Bado,mpaka combination ya wachezaji kukaa may be ni baada ya msimu mmoja msiposajili Tena,lakini kwa Sasa tunaomba mtusamehee,Simba ataendelea kudominate Tanzania Football,Simba oyeeereeee,ZANACO oyeeeeeee

    ReplyDelete
  9. Huyu kipa tuliambiwa anadaka hadi mishale, imekuwaje tena?

    ReplyDelete
  10. Ndio tuliambiwa anadaka Hadi aibu. Tuliambiwa hajui kufungwa anadaka Hadi upepo ��

    ReplyDelete
  11. Mikia kuna vibwetere wengi.
    KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amebainisha kwamba bado timu yake haijawa na muunganiko bora licha ya kwamba ilikuwa imeweka kambi nchini Morocco.

    ReplyDelete
  12. Mapovu rasmi, tuachieni yanga yetu

    ReplyDelete
  13. Utopolo mnatia aibu,
    Mmeshidiki kagame aibu, mechi za kirafiki aibu na bdo aibu itatawaka mpaka mwisho

    Nendeni mkafuatilie ya Morrisoni mpira ushawashinda porojo ndomnaweza

    ReplyDelete
  14. Huo ndio mpira,na hii ndio yanga,yanga ni ile ile mpira wao ni ule ule na matokeo yao ni yaleyale.kwa ufupi pole
    sana mtani huo ndio mpira acha kupiga porojo unapoteza muda mwingi sana na nguvu nyingi bila mafanikio nisalimie manara.

    ReplyDelete
  15. Hiyo saprais tuliyoahidiwa hatujaiona isipokuwa ile ya kucharazwa mabao kwa mechi zote mbili tena nyumbani mbele ya maelfu ya mashabiki waliokuwa na ukakika wa ushindi hata baada ya kuruhusiwa kuwatumia nyota waliojiunga tumu ya taifa

    ReplyDelete
  16. Eti Yanga kiroho safi juu ya kushindwa. Hakyna la kufanya ila kutamka hayo

    ReplyDelete
  17. Ingekua simba ndio kachapwa ungeona vichwa vya habari,ila timu ya wananchi hawaandiki vichwa vya kuifedhehesha timu wajinga sana yanga ila wanapaswa kujua mpira haupo kwenye vyombo vya habari wala midomoni,ushauri wa bure tengenezeni timu kwanza kwa muda wa miaka mitatu ndio mtakuja kufanya vizuri.yanga hakuna mpira pale ubabaishaji mwingi sana.poleni sana wananchi.

    ReplyDelete
  18. Imekaa hivi Kelvin Kapumbu awapiga pumbu utopolo

    ReplyDelete
  19. Asante Kapumbu kwa kuwapiga Pumbu hao Utopolo maana mtaani Leo tusi gefanya kazi

    ReplyDelete
  20. Kufungwa ktk matamasha haya huwa sio ajabu coz ni mechi za mwanzo wa msimu,,,hata Makolo miaka michache nyuma mlikula Tatu mtungi na Zesco toka huko huko Zambia

    ReplyDelete
  21. Usihesabu ya nyuma unaanza kusoma historia baada ya kushindwa, tulisbili surprise kumbe surprise yenyewe Nandy

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic