YANGA inaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ikiwa ipo nchini Morocco na imewajumuisha wachezaji wake wapya pamoja na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2020/21.
Miongoni mwa nyota waliopo kambini ni pamoja na Yacouba Songne ambaye ni namba moja kwa utupiaji msimu wa 2020/21 na Zawad Mauya.
Ni mabao 8 alifunga na pasi nne za mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao 12 kati ya 52 ambayo yalifungwa na timu hiyo.
Kwa wale wachezaji wapya ambao wapo kambini ni pamoja na Jesus Muloko ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Tuisila Kisinda ambaye anatajwa kuibukia Morocco.
Heritier Makambo ambaye aliwahi kucheza Yanga zama za Mwinyi Zahera naye amerejea tena kikosini.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa.
Hi yanga au team ya taifa congo ? Hawajiamini mwisho watasajiri hata waokota mipira congo yaani yanga bado wanampa nafasi simba kuchukua kombe maana wao bado wanatengeneza team labda waunde bendi ya muziki maana nimeona kwa kucheza wako vzr
ReplyDelete