August 18, 2021

 


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kila kitu kuhusu kambi na maandalizi ya msimu wa 2021/22 yanakwenda sawa.


Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu mpango kazi wa timu hiyo.



"Mzigo wa jezi upo na tutautambulisha wiki moja kabla ya siku ya Simba day. Mambo yanakwenda vizuri na kuanzia msimu ujao tutafanya kwa uzuri zaidi.


"Kuhusu kambi ya Simba iliyopo Morocco huko kila kitu kinakwenda sawa kuanzia kwa wachezaji wenyewe wanasema kuwa kambi ni nzuri," .


Simba inayonolewa na Gomes imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.


Septemba 25 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba v Yanga utakaokuwa ni wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Septemba 29.


Kambi ya Simba imejumuisha wachezaji wapya ikiwa ni pamoja na Duncan Nyoni, Abdul Samad, Peter Banda pia wapo wengine waliokuwepo msimu uliopita, Meddie Kagere, Said Ndemla,John Bocco.

3 COMMENTS:

  1. Si mliandika Ezekiel Kamwaga amefungasha vilago? Siyo msemaji tena wa timu ya Simba, sasa anatoa taarifa kama nani?

    ReplyDelete
  2. Watanzania kwa kulishana matango pori ni Hatar sana.simba nguvu moja hakuna kurudi nyuma.

    ReplyDelete
  3. Et kamwaga kasepa,, af mnaripoti taarifa zake....! Msiwe mnakurupuka kuandika udaku humu, muwe mnatoa taarifa zenye uhakika bhn!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic