September 7, 2021



KIKOSI cha Yanga ambacho kwa sasa kambi yake ipo kijiji cha Avic Town, Kigamboni unaambiwa dozi ni mara mbili kwa siku ikiwa ni lengo la kujiweka sawa kuelekea katika mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Yanga, ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Rivers United ya Nigeria  Septemba 12, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa awali.

Chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia imeelezwa kuwa utaratibu uliopo wa mazoezi ni mara mbili kwa siku ikiwa ni program ya asubuhi na jioni na wastani ni saa tano zinatumika sawa na dakika 300.

Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku ikiwa ni asubuhi na jioni.

"Ratiba ya mazoezi ni asubuhi na jioni huu ni utaratibu wa kawaida ambao klabu nyingi zenye mahitaji fulani zinafanya," .

Baada ya kete ya kwanza kimataifa kwa Yanga kukamilika Uwanja wa Mkapa Septemba 12 kibarua kingine ni kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Septemba 17, nchini Nigeria.


Chanzo:Spoti Xtra.


2 COMMENTS:

  1. Siyo kweli kutwa mala mbili for what,jamani Waandishi mna potosha hayo mazoezi mnayosemaga huwa ni ya soka kweli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tarehere 21 inkaribia ligi daraja la kwanza inakribia. CAS hoyeeee

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic