September 7, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Simba Day, Septemba 19 kushuhudia kikosi kazi na namna ambavyo watafanya uwanjani.

Raia huyo wa DR Congo huu unakuwa ni msimu wake wa pili kwa kuwa alikuwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kuanzia msimu wa 2020/21.

Nyota huyo alitupia jumla ya mabao 15 msimu uliopita akiwa ni namba mbili kwa watupiaji wote ndani ya ligi na Simba huku kinara akiwa ni nahodha wa Simba, John Bocco ambaye alitupia mabao 16.

Mugalu amesema:"Mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika siku ya Simba Day kwa kuwa ni siku ambayo itatukutanisha wachezaji na mashabiki kwa pamoja.

"Wanatakiwa kuja kwa wingi ili kuona nini ambacho tumewaandalia, kila kitu kipo sawa waje kwa wingi bila kukosa," amesema.

Kwa sasa kikosi cha Simba kimeweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Kwenye kilele cha Simba Day wanatarajia kucheza na moja ya timu ambayo imetwaa ubingwa wa Afrika zaidi ya mara nne na nafasi kubwa inapewa Al Ahly ile ya Misri.

2 COMMENTS:

  1. Mugali mwako huuinatakiwa ufunge zaidi ya bao 20 ndio nitakuelewa

    ReplyDelete
  2. Mugalu uko njema mwaka natabir kwa jinsi alivyoona anajua sasa ukubwa mechi zote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic