September 29, 2021


 LEGEND wa BongoFleva, Dully Sykes ‘Brotherman’ amesema kuwa Harmonize ni kijana wake kama walivyo vijana wake wengine na hana tatizo naye kama inavyochukuliwa na watu.

Nyota huyo ni Mwanapinduzi kwenye suala la muziki wa Tanzania kutokana na kazi zake nyingi kufanya vizuri na amekuwa ni mshauri kwa wasanii wengine kufanya kazi zao kwa ubunifu.

Kazi zake zimekuwa zikiishi na hata anapopewa nafasi ya kushirikishwa bado amekuwa akifanya poa jambo linalofanya azidi kuwe kwenye ramani ya muziki.

Kazi yake ya Bongo Fleva bado inaishi licha ya kuwa ni ngoma ya muda mrefu pia ile ya Hunifahamu bado inasumbua vichwa vya wengi.

Pia ngoma yake ya Dhahabu ni moja ya kazi nzuri na ilimpa mafanikio makubwa Afrika Mashariki na kati na duniani pia.

 Dully Sykes ameongeza kusema baadhi ya watu mitaani na mitandaoni ndio wanasababisha maneno na story zinazoendelea ila kwao hawana tatizo lolote na ikitokea kufanya kazi nyingine na Harmonize wataifanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic