MOHAMED Dewji, 'Mo', Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba ameweka wazi kuwa kwa sasa atabaki kuwa Mwanahisa ndani ya timu hiyo baada ya kukubaliana na Bodi kwamba anaweza kustep down, (kukaa pembeni) kwenye nafasi hiyo.
Mo amesema kuwa sababu kubwa ambayo imemfanya akajiengua ni kutokuwa na muda kwa kuwa amekuwa akisafiri mara kwa mara hivyo nafasi hiyo itakuwa mikononi mwa Salim Abdalah, 'Tryagain'.
Mo amebainisha pia mafanikio ambayo wameyapata kwa muda wa miaka minne ikiwa ni ile ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne pamoja na kuweza kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku akisistiza kwamba bado anaipenda Simba na yupo Simba.
Mmmmmh Simba ndo hvo tena mzimu wa yanga umehamia kwetu
ReplyDeleteWapigaji wengi!
ReplyDeleteMo kasoma alama za nyakati kaona hapo Simba mwaka huu ni shida tu
ReplyDelete