September 8, 2021

 


WAKATI kwa sasa ligi mbalimbali ambazo zimeanza Ulaya zikiwa zimesisimama kwa muda kutokana na timu za taifa kuwa na majukumu kwenye michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia tayari fukuto la tuzo ya ufungaji bora limeanza kushika kasi.

Kwa upande wa ligi inayoaminika kwamba inapendwa na kufuatiliwa na watu wengi duniani ambayo ni ile Ligi Kuu England staa wao ambaye anawakimbiza kwa sasa kwa kutupia mabao mengi ni Michail Antonio ambaye anakipiga ndani ya West Ham United ametupia mabao manne timu yake ikiwa imecheza mechi tatu.

Anafuatiwa na Bruno Fernandes staa huyu anakipa ndani ya Manchester United pamoja na Dominic Calvert-Lewin yupo zake ndani ya Everton hawa wametupia mabao matatumatatu kila mmoja.

Ligi nyingine ni ile ya La Liga ambayo haina mfalme wao wa muda wote Lionel Messi yupo zake ndani ya Ligue 1 huku kwenye ligi yao kinara ni Erik Lamella wa Sevilla, Angel Correa wa Atletico na Vinicius Junior wa Real Madrid nyota hawa wote wamecheka na nyavu mara tatutatu.


Ukija kwenye Bundesliga ni mnyama wao wa siku zote Roberto Lewandowski wa Bayern Munich jamaa katupia mabao matano huku timu yake ikiwa imecheza jumla ya mechi tatu anafuatiwa na Taiwo Awoniyi wa Union Berlin ni mabao matatu ametupia.

Sasa ile Ligue 1 ambayo Messi yupo akiwa amesepa na kijiji chake kutoka ndani ya Barcelona hapa ni kijana Kylian Mbappe ambaye anacheza na Messi ndani ya PSG,Mohamed Bayo ambaye yupo Clermont, Moussa Dembele anakipiga Lyon,Amine Gouiri yupo zake Nice na Dimitri Payer yupo zake Marseille hawa jamaa wote wamecheka na kamba mara tatutatu kwenye.

Pia kwa upande wa Serie A ambayo nayo mfalme wao Cristiano Ronaldo amesepa na sasa yupo England katika Klabu ya Manchester United huku kinara wao ni Ciro Immobile wa Lazio ametupia mabao manne na anafuatiwa na Jordan Veretout wa Roma ametupia mabao matatu.

Vita imeanza mapema huku kila mchezaji akifanya mambo yake katika kutimiza majukumu yake ni suala la kusubiri na kuona nani atakuwa nani mwisho wa msimu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic