UFALME wa mzawa Mbwana Samatta ndani ya Klabu ya Fenerbahche ulizimwa na kiungo huyu mshambuliaji Mesut Ozil ambaye anaihusudu jezi namba 10 jambo lililofanya Samatta abadilishiwe namba ya jezi zama alipokuwa ndani ya timu hiyo.
Umri wake wa miaka 32, Ozil ambaye ni raia wa Ujerumani ameweza kuwa na furaha kwa kutwaa mataji mbalimbali jambo ambalo huwa ni ndoto za wachezaji wengi duniani.
Taji la Kombe la Dunia ambalo alitwaa akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 2014 ni moja ya jambo ambalo linaikuza thamani yake pamoja na kuendelea kupambana muda wote.
Kabatini ana tuzo moja kubwa ambayo ni muhimu pia kwake ni ile ya mchezaji bora wa mwaka kwa msimu wa 2014/15 ilikuwa ni kwa taifa la Ujerumani na wakati huo timu yake ya taifa ilitwaa Kombe la Dunia.
Rekodi zinaonyesha kuwa ametwaa mataji mengi akiwa ndani ya kikosi cha Arsenal ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta nayo ni mataji sita.
Mataji hayo manne yote ni ya FA Cup ambapo ilikuwa ni mwaka 2014,15,17 na 20 pia alishinda taji la English Super Cup mara mbili ilikuwa ni 2015 na 16.
Ni Real Madrid ya Hispania huko alicheza jumla ya mechi 105 na kutupia mabao 19 huku ndani ya Arsenal kuanzia 2013/2021 alicheza jumla ya mechi 184 na kutupia mabao 33 ikiwa ni timu ambayo alicheza mechi nyingi zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment