September 3, 2021


 ALIYEKUWA mshambuliaji wa Al Wahda FC ya nchini Libya, Adam Adam amefanikiwa kujiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Adam kabla ya kujiunga na Polisi Tanzania alikuwa anakipiga katika Klabu ya Al Wahda FC ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Tanzania.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa timu hiyo, Juma Hassan amethibitisha kuwa ni kweli wamewasajili wachezaji hao ili kuweza kuongeza nguvu katika kikosi chao cha msimu ujao.


Aliongeza kuwa, katika kikosi chao zilibaki nafasi mbili lakini moja tayari imepata mwenyewe ambaye ni kipa Metacha Mnata aliyekuwa anachezea Yanga katika msimu uliopita na taarifa za usajili wake wote utajulikana rasmi na watamtangaza rasmi.

 

“Malengo yetu kama timu ni kufanya usajili mzuri kwa ajili ya msimu ujao na ndio maana tumewasajili wachezaji hao na wengine ambao tumewasajili kutokana na uhitaji wa timu.

 

“Tumemsajili Adam kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongeza nguvu katika kikosi chetu cha msimu ujao lakini pia Metacha ambaye tutamtangaza  pamoja na wachezaji wetu wote wapya.”


Tayari Metacha ametangazwa kuwa mali ya Polisi Tanzania hivyo ataanza changamoto mpya msimu wa 2021/22 akiwa katika kikosi hicho kinachonolewa na Malale Hamsini.


Hivyo kwa msimu mpya Polisi Tanzania nao hawatakuwa wa mchezomchezo kutokana na usajili waliofanya ikiwa utajibu wataendelea na kasi yao ya msimu uliopita.


Ikumbukwe kuwa 2020/21 walisepa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 34 na ilikuwa nafasi ya 6.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic