September 29, 2021

 


BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kubanwa mbavu mbele ya Biashara United wamebainisha kuwa walipambana kusaka ushindi ila haikuwa bahati yao.


Katika mchezo wa kwanza wa msimu wa 2021/22 uliochezwa Uwanja wa Karume,Mara, mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba.

Unakuwa ni mwanzo wa kipekee kwa Simba ambao msimu wa 2020/21 mchezo wao wa kwanza walishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ihefu ambayo kwa sasa inashiriki Championship ila jana Septemba 28 waligawana pointi mojamoja na Biashara United.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda licha ya kupambana kusaka ushindi.

"Haikuwa bahati yetu, wachezaji walipambana kwa namna ambavyo wanaweza lakini tumeshindwa kushinda, matokeo tunayachukua tutafanya kazi mchezo ujao kwani ligi inaanza na kila timu inahitaji ushindi,".


Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Dodoma Jiji inayonolewa na mzawa Mbwana Makata. 


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba Mosi, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Ikiwa imetoka kulazimisha sare na kugawana pointi moja inakutana na Dodoma Jiji iliyotoma kuwanyoosha Ruvu Shooting bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

3 COMMENTS:

  1. Simba hii team yangu inanipa mashaka.Nafikiri last season Simba hajawahi kucheza mechi tatu mfululizo asipate angalau goli moja.Juzi watu walilalamika kwamba Mugalu anakosa magoli ya wazi, waanze Bocco na Kagere kocha kawaanzisha na hakuna walichokifanya zaidi ya Bocco kung'ang'ania kupiga kupiga penalt ili awe mfungaji bora wakati kwenye team yetu mtaalam wa kupiga penalt anajulikana ni Erasto Nyoni.Mimi nafikiri wana Simba wenzangu kuna kitu kimejificha nyuma ya Simba au inabidi kocha abadili mbinu uwanjani za kucheza, maana jana nilishangaa kutomuanzisha Pape Sakho ambaye ana kasi na wote tumeshuhudia alivyoingia alivyobadili mpira na kusababisha penalt.Inabidi benchi la ufundi lipange kikosi kulingana na uwezo wa wachezaji na cyo kusikiliza kelele za mashabiki, kwani wao ndiyo wanakaa na wachezaji kwenye training Camp, wote jana tumeona umuhimu wa Mugalu maana Bocco na Kagere wamechemka kabisa labda sababu ya Umri.Vilevile Israel Mwenda ni mzuri ila inabidi apewe nafasi zaidi.Wawa na Shomary Kapombe inabidi waanze kupumzishwa, tumeona mechi ya tangia Tp Mazembe na Yanga jinsi Shomary Kapombe anavyochemka.Mwisho wana Simba tusiumie sana kwani kufungwa siyo mwisho wa dunia, bado tuna nafasi ya kupata team madhubuti kama benchi la ufundi halitaingiliwa ovyo.Naamini mechi ya Dodoma tutashinda ila inabidi wachezaji wenye kasi kama Morrison, Pape na Peter Banda waanze ili tutengeneze threat chances nyingi golini

    ReplyDelete
  2. Simba hii inatia mashaka kidogo sidhani hata mechi na Gallax FC ya Botswana kama tutatoboa, maana nimeshangaa Simba kucheza mechi tatu mfululizo asipate angalau goli moja hata kama mechi tumefungwa.Nafikiri benchi la ufundi inabidi lifanyie kazi mapungufu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo imeonekana kuwa butu katika mechi tatu mfululizo.Jana hatukutengeneza threat chance zaidi ya alipongia Pape Sakho na kusababisha penalt ambayo Bocco alilazimisha apige ili awe mfungaji bora.Nafikiri mdau hapo juu upo sahii, Simba inakosa watu hatari wa kusababisha mashambulizi hatari kwenye lango la adui kama walivyokuwa wakifanya wakina Chama na Missquine.Nafikiri ni muda wa Morrison, Pape Sakho na Peter Banda kuanza ili kutengeneza threat chances golini.Bocco na Kagere walikuwa wanabebwa na wakina Luis na Chama ila uwezo wa kutafuta mipira wenyewe hawana.Nafikiri kocha asipobadilisha mbinu za kuwaanzisha mawinga wenye speed yale magoli 78 tutayasikia kwenye upande wa Zungu.Wana Simba tusikate tamaa kwa sababu ndiyo kwanza league imeanza hata wale wa upande wa pili mwaka jana walianza na tambo nyingi lakini walipofika round ya nane Coastal Union alifanya yake na wakaanza kupotezana mazima.Naamini tutaimarika siku hadi siku

    ReplyDelete
  3. Kuwataja wachezaji ambao hawapo nao ni ushamba! Yaani Simba haiwezi lolote bila Chama na Luis?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic