LEO Septemba 29, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba,Kagera. Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli amebainisha kuwa wapo nyota ambao watakosekana katika mchezo wa leo kutokana na sababu mbalimbali.
Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Said Ntibanzokiza, Mapinduzi Balama pamoja na Mukoko Tonombe pia ameweka wazi kwamba wanahitaji ushindi mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa wana rekodi nzuri wakiwa Kaitaba.
0 COMMENTS:
Post a Comment