September 7, 2021

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen leo Septemba 7 imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar. 

Ni katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa Mkapa na hakukuwa na mashabiki kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Walioruhusiwa kuingia walikuwa ni Waandishi wa Habari ambao nao ilikuwa ni kwa idadi maalumu pamoja na viongozi na wasimamizi ambao nao pia wote walipaswa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Mabao ya Stars kwenye mchezo wa leo uliokuwa na ushindani yalifungwa na Erasto Nyoni dk 2, kwa mkwaju wa penalti, bao la pili lilipachikwa na Novatus Dismas dk ya 26 ilikuwa ni kipindi cha kwanza na yote yalirudishwa kipindi cha kwanza na ubao ulisoma Tanzania 2-2 Madagascar.

Kwa Madagascar ni Rakotoharimalala dk ya 36 na Fontaine dk 45 kwa pigo huru akiwa nje ya 18. 


Kipindi cha pili baada ya mapumziko vijana wa Stars waliweza kujipanga na kusaka ushindi kwa juhudi. 

Pasi ya upendo kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta ilikutana na miguu ya Feisal Salum ambaye alipachika bao la ushindi ilikuwa ni dk ya 52.

Ushindi huo unaifanya Stars kuongoza kundi J ikiwa na pointi zake kibindoni 4 sawa na Benin zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi mbili.

Tofauti ni idadi ya mabao ya kufunga ambapo Tanzania imefunga mabao manne huku Benin ikiwa imefunga mabao matatu.

2 COMMENTS:

  1. Kama kawaida ya wachezaji wetu wanapotangulia kwa idadi nzuri ya mabao basi hujiona wameshamaliza mechi na kuanza kuleta nyodo,sijui watajifunza lini kuamini kwamba ushindi unapatikana baada ya filimbi ya mwisho.Walianza kuleta nyodo na kuacha kucheza kwa nguvu baada ya kuongoza magoli mawili matokeo yake magoli yakarudishwa na kujikuta wanatumia nguvu nyingi kutafuta ushindi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic