September 5, 2021


 MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Bara wanatamba kitaa kwa sasa na uzi wao mpya wa msimu wa 2021/22 ambao ulizinduliwa hivi karibuni Mlimani City.

Mbunifu wa uzi huo ni mzawa Sheria Ngowi huku akiweka wazi kwamba kila nembo iliyotumika katika uzi huo ilizingatia mahitaji ya soko pamoja a uchaguzi wa rangi yenye ubora.

Uzi ambao umeonekana kupendwa na kuuza kwenye maduka ni ule wa rangi ya njano na picha za watu kwa mbali ambazo Ngowi amesema kuwa alizingatia maana halisi ya 'Sisi Tuna Watu'.

Hata uzi wao ule wenye rangi ya kijani ambao ni uzi wa nyumbani ni miongoni mwenye muonekano pia wa picha hizo za 'Sisi Tuna Watu'.


7 COMMENTS:

  1. Ubunifu mzuri sana, umetumia 'theme' iliyopo sio wao 'copy and paste' kama makoro fc

    ReplyDelete
  2. Kama wao wanawatu wasinge sotea ubingwa kwa mwaka wa tano huu sasa..wakisema wao wanamisukule sawa.

    ReplyDelete
  3. Kwani hakuna kipindi nao walichukua minne...na bado ni mabingwa wa kihistoria?

    ReplyDelete
  4. Nachekaaaa maana hii yote ni kujifariji na bado ulimbukeni wenu mnalipwa tzsh 1300 kwa kila jezi na kwa mwaka mnalipwa milioni 45.Mjitafakari na ulimwengu wa kisasa unavyoenda.

    ReplyDelete
  5. Wewe unayecheka kiasi kinacholipwa weka zako na kamuulize MO hayo matangazo juu ya jezi analipa sh ngapi,Kama tu maudhui ya Tv Azam wamelipa 45 na je anayeniliki Timu maisha kwa B20 je????

    ReplyDelete
  6. Na ndani ya watu hao mazezeta na mataahira ndio wamechukua nafasi kubwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic